Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mh. Majid Mwanga ametoa siku tatu kwa uongozi wa kitongoji na kijiji cha Madoto kuwasilisha muhtasari wa kikao walichokaa na wananchi na kuridhia kuuzwa kwa shamba la kijiji lenye ukubwa wa ekari 50 ambalo limekuwa likiwa likilalamikiwa na wanakijiji kwamba limeuzwa kinyemela bila ushirikishwaji na fedha zake hazijulikani zilipo.
Mh. Mwanga ametoa agizo hilo Agosti 26 mwaka huu kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya Madoto wakati akisikiliza kero zinazowakabili wananchi ambapo amesema kuwa kumekuwa na tabia kwa baadhi ya viongozi wa chini kuuza ardhi bila ya kufuata sheria za ardhi, hali inayochochea kuibuka kwa migogoro ya ardhi na kwamba endapo itabainika mihutasari haitakuwa na saini viongozi wote walioshiriki kwenye mauziano ya shamba hilo watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Katika hatua nyingine ametoa onyo kwa wafugaji ambao wanajihusisha na ulishaji wa mazao ya wakulima kuacha mara moja na watakaokiuka onyo hilo Serikali ipo macho na haitosita kuwashughulikia kwa mujibu wa sheria na kwani wafugaji na wakulima ni makundi yanayotegemeana kimaisha na katika kukuza uchumi wa nchi, hivyo nidhamu lazima iwepo kwa pande zote.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa