Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Alhaji Majid Mwanga amesema kuwa Wilaya ya Kilosa ina upungufu wa madawati takribani elfu 14 na 400 na kusema kuwa suala hilo kwa kiasi kikubwa linamnyima usingizi hivyo ameahidi kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa ili kuja na mkakati wa kubuni njia ya kutatua changamoto hiyo kwa spidi kubwa.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema hayo Juni 21 mwaka huu (2022) wakati wa kikao cha kusikiliza hoja za CAG kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya Msingi Madaraka wilayani hapa.
Mh Alhaji Majid ametolea mfano shule ya msingi Dumila juu pekee ina upungufu wa madawati takribani 1873 huku shule ya Msingi Mtumbatu watoto 1200 wanakaa chini kutokana na upungufu huo wa madawati,sambamba na hayo pia amebainisha kuwepo na upungufu wa Zahanati na kwamba huduma za afya bado haziridhishi.
Amesema kuwa Sera ya Serikali ni kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na Zahanati lakini katika maeneo mengi kuna changamoto ya kukosekana kwa huduma hiyo huku akimuomba Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Martin Shigella kushirikiana Wilaya kumaliza changamoto hiyo ambayo inahusisha maisha ya watu.
Aidha Mkuu wa Wilaya Alhaji Mwanga amewataka Waheshiwa Madiwani kushiriki kikamilifu katika kampeni ambayo ameianzisha ya kujenga zahanati kwa kuku kwa kuendelea kuhamashisha wananchi kuchangia ujenzi hususan katika kipindi hiki cha mavuno.
Awali Mkuu huyo wa Wilaya aliipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa kwa kupata hati safi kwa miaka nane mfululizo na kuahidi kushirikiana na timu ya Wilaya ili kuendeleza mema yaliyofanyika kwani itakua aibu kubwa kwa wote kama hati safi ikikosekana miaka ijayo.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa