Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Shaka Hamdu Shaka amekabidhi pikipiki tano (5) aina ya boksa kwa maafisa mifugo kutoka kata za Magomeni, Masanze, Kilangali, Madoto na Parakuyo kwa ajili ya kurahisisha utendaji kazi.
Akikabidhi pikipiki hizo zilizotolewa na wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi Februari 1, 2024 kwa maafisa ugani hao amewataka Kwenda kuzitunza na kuzifanyia kazi iliyokusudiwa ambapo amesema pikipiki hizo zitawasaidia kurahisisha usafiri katika maeneo yao ya kazi ikiwa ni jitihada ya kuhakikisha wanafikia wafugaji na kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo migogoro ya wafugaji na wakulima.
DC Shaka ameongeza kuwa katika sekta ya kilimo na mifugo kumekuwa na changamoto mbalimbali ya ufanyaji wa tathimini ya mazao na kwamba pindi yanapoliwa au kuharibiwa na mifugo hivyo maafisa hao wanapaswa kuboresha utendaji kazi wao na kuhakikisha wanatenda haki pindi wanapofika eneo la migogoro.
Pia amewataka watumishi hao kushirikiana na kufanya kazi kwa uadilifu na kujiepusha na masuala mazima ya rushwa kwani ni ukiukwaji wa sheria.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa halmashsuri ya Wilaya ya kilosa Ndg. Michael J Gwimile ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuwaletea vitendea kazi hivyo kwa maafisa ugani hao na kusema kuwa itaongeza ufanisi katika maeneo yao ya kazi hususan katika suala zima la ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri katika sekta hiyo.
Aidha Mkuu wa divisheni ya kilimo,uvuvi na mifugo wilayani kilosa Ndg. Elia Shemtoe amesema pikipiki hizi zitakuwa chachu na kuwafanya watumishi hawa kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa kwa kuyafikia maeneo ambayo awali yalikuwa hayafikiki kirahisi kutokana na uchache wa pikipiki hizo.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa