Mkuu wa wilaya ya Kilosa Mhe. Shaka Hamdu Shaka ameipongeza serikali ya awamu ya sita kupita Wizara yUchukuzi kwa kuufufua uwanja wa ndege wa kilosa na kuwataka wananchi kutumia fursa hiyo ya usafiri na usafirishaj.
Pongezi hizo amezitoa leo wakati wa mapokezi ya ndege ya kwanza kutua katika uwanja huo, huku akifafanua kuwa lengo la serikali ni kuzifungamanisha sekta mbalimbali za kiuchumi kama vile utalii, kilimo na usafirishaji ili kukuza biashara za kikanda
Mhe. shaka amesema kuwa lengo la serikali ni kuupanua uwanja huo ili uweze kuhudumia ndege kubwa ikiwa kwa sasa serikali inajipanga kufanya tathimini ya ujenzi wa uwanja huo.
Aidha Mhe. Shaka amewataka wananchi wa eneo hilo kuutunza uwanja huo ikiwa ni pamoja na kuacha kufanyia shughuli za kibinadamu kama vile ufugaji.
Ndege hiyo aina ya 5LSB imetengenezwa hapa Tanzania na Kampuni ya Africa Airplane Limited yenye makazi yake Mkoani Morogoro
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa