Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka H Shaka kupitia kikao cha Baraza la Madiwani la kujadili na kupitisha rasimu ya mpango wa bajeti kwa mwaka wa Fedha 2023/2024 ametoa rai ya kumalizwa kwa migogoro ya wakulima na wafugaji, kwa kila mmoja kuwajibika eneo lake kwa kuhakikisha haki inatendeka kwa wakulima na wafugaji badala baadhi ya ya watendaji wa kata na vijiji pamoja na madiwani kuwa wanufaika wa migogoro hiyo, kwani kuwa wanufaika migogoro hiyo itapelekea kutoisha.
Shaka amesema hayo Februari 16 mwaka huu ambapo amesema kuwa katika uongozi wake hatakubali kumvumilia kiongozi asiye mwadilifu na kuwa chanzo cha migogoro kwa kuendekeza rushwa bali kila mmoja ahakikishe anafuata sheria, kanuni na taratibu za kimaadili kila mmoja katika eneo lake, huku akisisitiza kuwepo kwa juhudi za makusudi katika kubuni vyanzo vipya vya mapato pamoja na usimamizi wa ukusanyaji wa mapayto hayo, ambapo ametaka fedha yoyote inayokusanywa kupelekewa benki kama zilivyo taratibu badala ya kuanza kuzitumia bila kufuata utaratibu.
Aidha katika baraza hilo Shaka ameishukuru serikali ya awamu ya sita ckwa kuwatazama watendaji wa kata kwa jicho la tatu na kuwapatia pikipiki ambazo anaamini zitawasiadia katika utendaji wa majukumu yao ya kila siku kwani uwepo wa pikipiki hizo unatarajiwa kutatua changamoto ya usafiri hususani kwenye maeneo yasiyofikika kwa urahisi kutokana na kukosa usafiri.
Katika kikao hicho cha baraza la madiwani limepitia mapitio ya bajeti ya mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2021/2022 na kipindi cha Julai- Desemba 2022 kwa mwaka wa fedha 2022/2023, lakini pia limepitisha kwa pamoja Rasimu ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri kwa mwaka wa Fedha 2023/2024 ya shilingi bilioni 61, 579,299,755
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Mh. Wilfred Sumari amesema kuwa Serikali ya Wilaya ya Kilosa ilishatoa maelekezo kila kijiji na kata kufanya utambuzi yakinifu wa wa mifugo na wafugaji kwa kijiji na kata, sambamba na kuunda kamati za usuluhishi pamoja na kuondoa mifugo ambayo imeingia bila kibali lakini baadhi ya viongozi wa kata wamekuwa wakikaidi agizo hilo kwa kutolitekeleza kwa wakati.
Sumari amesema ni muda muafaka sasa wa kuanza kuchukua hatua kwa wale wote ambao hawajatekeleza maagizo hayo na kusababisha wilaya kuendelea kuwa katika migogoro ambayo kwa kiasi kikubwa inaweza kuzuilika kwa kila mmoja kutekeleza majukumu yake kwa wakati kwa kufuta sheria, taratibu na kanuni
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa