Mkuu wa wilaya ya Kilosa Mh. Shaka Hamdu Shaka amewataka viongozi wa ngazi mbalimbali katika ngazi ya kata na vijiji ili kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi katika katika maeneo yao ili kutoa huduma bora inayokusudiwa na Serikali..
Mh Shaka amesema hayo Mei 18 mwaka huu wakati wa kikao cha baraza la madiwani ikiwa ni robo ya tatu ambapo amesisitiza usomwaji wa taarifa za mapato na matumizi kwenye vikao stahiki kwenye maeneo yao ili kuleta uwazi juu ya matumizi ya fedha zinazoletwa kwaajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.
Sambamba na hayo Mh. Shaka ameipongeza Serikali Kuu kwa kuipatia Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa shilingi Bilioni 2,025,800,000 kupitia mradi wa kuboresha Elimu ya Awali na Msingi Tanzania(BOOST) ambapo fedha hizo zitatumika katika kujenga miundombinu mbalimbali ikiwemo ujenzi wa shule mpya, ujenzi wa vyumba vya madarasa ya mfano kwa elimu ya awali, ujenzi wa madarasa kwa elimu msingi na matundu ya vyoo mashuleni katika kata mbalimbali.
Aidha, Mh. Shaka amewataka wataalam kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kuongeza mapato ya ndani yatakayosaidia katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hususan kwenye sekta ya elimu, afya na maji huku akisisitiza kubuni mikakati itayoboresha uhifadhi wa mazingira, usafi wa mazingira, utunzaji wa vyanzo vya maji na kutatua migogoro ya wafugajji na wakulima huku akisisitiza kuwepo kwa ushirikiano thabiti ili kutekeleza mikakati hiyo ambayo italeta mafaniko makubwa na ameahidi ushirikiano wa kutosha katika kuboresha mikakati na maendeleo ya Wilaya ya Kilosa.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa