Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Comrade Shaka H. Shaka amewataka walimu wakuu wote wa shule za sekondari kushirikiana na viongozi wa kata zote ikiwemo madiwani, watendaji wa kata na vijiji, wenyeviti pamoja na wazazi kuhakikisha wanafunzi wote wanaostahili kuanza kidato cha kwanza wanaripoti shuleni na kuanza masomo haraka iwezekanavyo.
Agizo hilo limetolewa Januari 09/01/2024 wakati akifanya ziara ya ufatiliaji mapokezi ya kaguzi wa mahudhurio ya wanafunzi walioripoti shule na kuanza masomo hususani kwa kidato cha kwanza, elimu ya awali na darasa la kwanza ambapo ametaka viongozi wa kata na vijiji vyote kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha wanafunzi wote wanaripoti na kuanza masomo ili watoto wote waweze kupata elimu inavyostahiki.
Shaka katika ziara yake ametembelea shule ya msingi na sekondari Parakuyo na shule ya sekondari Mkulo ambapo ametoa onyo kwa mzazi au mlezi yoyote atakayebainika kumtorosha mtoto hususani wa kike kwa lengo la kumuozesha kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake,huku akisisitiza wazazi au walezi kuacha mara moja tabia ya kufanya uhamisho feki ambapo kila uhamisho utafuatiliwa na ikibainika kuwa ni feki hatua stahiki zitachukuliwa kwa yoyote atakayehusika kwani tayari kuna baadhi ya wazazi wameanza kupokea mahari jambo ambalo limeshaanza kufanyiwa kazi na kuwa Serikali haitosita kuchukua hatua kwa mzazi atakayebainika kutaka kuhujumu upatikanaji elimu wa watoto.
Ujenzi wa hostel kwa ajili ya wanafunzi
Aidha ameuagiza uongozi wa kata ya Parakuyo kushirikiana na Idara ya ardhi kuhakikisha ifikapo tarehe 15/01/2024 eneo la mipaka ya shule ya sekondari Parakuyo inapimwa na kuainishwa vizuri ili kuepusha migogoro ya watu kuvamia maeneo ya Serikali huku akimshkuru Mheshimiwa rais Dkt. Samia suluhu Hassan kwa zaidi ya shilingi bilioni 3.5 zilizoelekezwa katika sekta ya elimu ambapo pia amewashukuru wabunge wa majimbo yote mawili Kilosa na Mikumi kwa ushirikiano na juhudi ambazo wamekuwa wakizifanya ili kuiletea Kilosa maendeleo.
Naye Katibu Mwenezi Jafari Kunambi kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kilosa amewataka viongozi wote wa CCM ndani ya kata zao kuendelea kuhamasisha jamii wanazoishi nazo kuona umuhimu wa elimu ili watoto wote waweze kupata elimu huku akitaka viongozi ngazi ya kata kuwa wepesi kutatua migogoro kwa wakati katika maeneo yao kwani kuna migogoro ambayo ipo ndani ya uwezo wao wanayopaswa kuitatua badala ya kusubiri viongozi wa ngazi za juu.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Parakuyo Mh Ibrahim Kalaita ameiomba Serikali kupitia mradi wa BOOST kuongeza shule nyingine ya msingi katika kijiji cha Mkata Station ili kuwapunguzia adha ya wanafunzi ya kutembea umbali mrefu, kwani kwasasa wanafunzi wa kijiji cha Mkata wanatumia shule ya msingi Parakayo ambayo kwasasa imekuwa na wanafunzi wengi.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa