Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Shaka H. Shaka amewaasa Maafisa Ugani Kilimo Wilaya kuwasaidia wananchi kufanya kilimo chenye tija ili kupata matokeo chanya na kuvitumia vyema vitendea kazi hivyo walivyokabidhiwa katika utekelezaji wa majukumu yao.
Mhe. Shaka ametoa wito huo 26 Septemba, 2024 kwa Maafisa Ugani kilimo Wilaya katika hafla ya kuwakabidhi vishikwambi 93 na magwanda 93 Maafisa hao ambapo Mhe. shaka amesema imani ya wananchi ni kuona mabadiliko na kusisitiza kuwa vitendea kazi hivyo vitakwenda kuwa kichocheo kwa kufanya kazi zaidi ili kuleta matokeo chanya kwenye sekta ya Kilimo.
Mhe. Shaka ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kupitia Wizara ya Kilimo kwa kutenga fedha kwa ajili ya Maboresho katika Sekta ya Kilimo ambapo asilimia kubwa wilayani hapo uchumi wake unategemea Kilimo.
Naye Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Elia Shemtoi amesema vitendea kazi hivyo ambavyo ni vishikwambi 93 na magwanda 93 vitarahisisha utekelezaji wa majukumu yao kwa kuwasadia wakulima ambapo Vishikwambi hivyo vitatumika katika kuchukua majira ya nukta lakini pia vitasaidia katika kupata orodha ya wakulima kupitia mfumo wa kuwasajili kupitia vishikwambi hivyo.
Shemtoi amesema kuwa taarifa za Mkulima zitaweza kusomeka katika mfumo pia vishikwambi hivyo vitaweza kuonesha taarifa ya utendaji kazi wa kila Afisa Ugani Kilimo katika maeneo yao wakati wa utekelezaji wa majukumu yao hivyo amewasihi kuvitunza na kuvithamini vitendea kazi hivyo.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa