Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe Shaka Hamdu Shaka amewataka Viongozi wa ngazi zote kuhamasisha na kuhabarisha Wananchi juu ya uwepo wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotajariwa kufanyika Novemba mwaka huu ili waweze kujitokeza kwa Wingi katika kushiriki kuanzia kujiandikisha mpaka kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
Mhe. Shaka amesema hayo 29 Agosti, 2024 wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani wa kupitia na kujadili Taarifa mbalimbali za utekelezaji wa Shughuli za Halmashauri kwa kipindi cha Robo ya nne (April-Juni) kilichofanyika katika Ukumbi wa FDC Ilonga,ambapo amewataka viongozi hao kuhamasisha Wanawake na Watu wenye ulemavu watakaokuwa na sifa za kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi katika Vijiji na Vitongoji kuchukua fomu na kuomba nafasi za uongozi.
Amewataka Wahe. Madiwani kutumia Mikutano yao ya Hadhara kuwahamasisha Wananchi kujitokeza na kutumia haki yao ya Kidemokrasia ya kuchagua Viongozi wa Vijiji,Vitongoji na Mitaa na Kusema kuwa katika uchaguzi huo hali ya Usalama na Amani itazingatiwa ili uwe Dira na Kioo cha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 wa Rais,Wabunge Pamoja na Madiw
Mhe. Shaka amesema kuwa Ustawi wa Mwananchi Wilayani Kilosa unategemea Busara za Baraza hilo hivyo amewaasa kila mmoja kwa nafasi yake ahakikishe malengo yaliyowekwa yanafikiwa kwa manufaa ya wana Kilosa na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande mwingine amemshukuru Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri na Baraza lake la Wahe Madiwani, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri na Timu ya Menejimenti kwa ushirikiano unaoendelea kuoneshwa katika mambo mbalimbali ya Maendeleo, na pia kufanikisha Ziara ya Kikazi ya Mhe Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Wilayani Kilosa na kwamba Ziara hiyo imekuwa kielelezo kikubwa cha Umoja na Mshikamano kati ya viongozi wa ngazi zote za Wilaya.
Amesema kuwa ni matumaini yake kuwa katika Zoezi zima la uchaguzi Umoja na mshikamano huo utaimarika maradufu.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa