Mkuu wa wilaya ya Kilosa Mhe. Shaka Hamdu Shaka amewataka wananchi wa Kata ya Masanze kudumisha amani na mshikamano baina ya wakulima na wafugaji kwani shughuli zao zinategemeana.
Mhe. Shaka ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi uliofanyika katika kijiji cha Changalawe kilichopo kata ya Masanze june 26, 2024
Amewasisitiza kuilinda amani iliyopo ili shughuli za kiuchumi ziweze kuendelea kwani bila amani si mkulima wala mfungaji watakofanya shughuli zao kwa utulivu.
Akijibu kero za wananchi wa kijiji hicho, Mkuu wa wilaya ameitaka familia ya mfugaji anayejulikana kwa jina la Losela ambaye ameonekana kuwa kero kubwa kwa wakulima kuondoka kwenye maeneo aliyoyavamia ndani ya siku kumi na nne ili kuleta amani ndani ya kijiji hicho.
Wakielezea kero zao, wananchi wamemtaja mfugaji huyo kuwa kero kwa kulisha mifugo kwenye mazao yao huku wengine wakipigwa na kujeruhiwa na mfugaji huyo pindi wanapokuwa wanaizuia mifugo yake kuingia mashambani kwao.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa