Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe.Shaka Hamdu Shaka amewashukuru Waislamu na wananchi wote kwa ujumla Wilayani humo kwa kutunza Amani, umoja na mshikamano katika kipindi chote cha mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kutaka hali hiyo kuendelea.
Shaka amayasema hayo 31 Machi 2025 wakati akitoa salamu za sikukuu ya Eid El-Fitr kwa Wananchi wa Kilosa akiwa katika shule ya Msingi Mazinyungu baada ya kukabidhi Msaada kwa watoto wenye mahitaji maalumu waliopo shuleni hapo ikiwa ni zawadi Maalum ya Eid El Fitr ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dokta Samia Suluhu Hassan kwa Watu wenye mahitaji maalum ambapo kwa Wilaya ya Kilosa zawadi hiyo imetolewa kwa Watoto wenye uhitaji Shule Msingi Mazinyungu na Kituo cha Kulelea yatima Dumila.
Akikabidhi msaada huo ikiwemo sukari, mchele, juice, unga wa ugali, mbuzi na mafuta ya kupikia na ya kupakaa Shaka amesema kuwa ametoa msaada huo kwa watoto hao ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Sikukuu za Eid El-Fitr na kuwafanya watoto hao kufurahi kwa pamoja.
Pamoja na mambo mengine Mheshimiwa Shaka amewataka wananchi kuendelea kuhurumiana na kupendana huku wakijiandaa kushiriki kikamilifu katika uchaguzi Mkuu wa kuchagua Madiwani, Wabunge na Rais unaotarajiwa kufanyika mwaka huu 2025.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa