Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Ndg. Michael Gwimile amewataka Watumishi na Wananchi Wilayani Kilosa kujenga Utamaduni wa kusafisha mazingira yao mara kwa Mara.
Ametoa rai hiyo wakati wa zoezi la kusafisha mazingira lililofanyika eneo la makao makuu ya Halmashauri (bomani) 1 Juni, 2024 ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani yatakayoadhimishwa 5 Juni 2024.
Amesema kuwa Halmashauri itaweka utaratibu kwa watumishi wake kushiriki zoezi la usafi wa mazingira wa pamoja kwa siku moja kila ifikapo mwisho wa wiki ili wananchi waige utamaduni huo wa kufanya usafi katika maeneno yao.
“…Kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani, tumeamua leo siku ya Jumamosi tuje kufanya usafi na hili sisi tunalitumia kama motisha na kila mwisho wa wiki tutakuwa tunafanya usafi ili mwisho wa siku utaratibu huu tuuhamishie kwenye jamii”
Zoezi hili limefanywa na watumishi mbalimbali wanaofanya kazi katika ofisi kuu za Halmashauri ambapo shughuli tofauti tofauti za usafishaji wa mazingira zimefanyika ikiwa ni pamoja na ufyekaji wa nyasi, kufagia mazingira pamoja na ukusanyaji wa taka.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa