Waganga wafawidhi kutoka vituo vya Afya, zahananti pamoja na wahasibu wa vituo hivyo wametakiwa kuhakikisha wanatekeleza agizo la kununua vifaa stahiki kwa ajili ya kufunga mfumo wa GoTHOMIS katika vituo vyao vya kazi hususani katika vituo vya Afya na zahanati ambazo hazijatekeleza agizo hilo.
Agizo hilo limetolewa Novemba 16, 2023 na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Ndg. Kisena Mabuba wakati wa kikao kazi kilichoshirikisha waganga wafawidhi wa vituo vya afya na zahanati pamoja na wahasibu wa vituo hivyo ambapo amesema kuwa kila mmoja atekeleze agizo hilo ili kazi ziweze kufanyika kwa njia ya mfumo lakini pia itasaidia kutopoteza mapato.
Aidha amewataka watumishi hao kuacha ubinafsi kwa kuhakikisha wanalinda kazi zao kwa kufanya majukumu yao inavyostahiki kwani ni watumishi wa umma ambao wanapaswa kuzingatia uwajibikaji kwa kutoa huduma nzuri kwa watu wanaowahudumia, huku akisisitiza suala la usimamizi wa matumizi sahihi ya fedha za Serikali pamoja na miradi inayotekelezwa katika maeneo yao.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa