Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya nne ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Kayanza Pinda ametoa wito kwa waandaaji wa maonesho ya wakulima(Nane Nane)kuyafanya maonesho hayo kuwa na tija kwa wakulima na nchi mzima kwa ujumla.
Wito huo ametoa Agosti 4, 2022v wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho hayo katika viwanja vya Mwl. Nyerere mkoani Morogoro kwa kanda ya Mashariki ambapo amesema ili kuwa na faida kwa wananchi inahitaji tathmini ya kila mwaka mara baada ya maonesho ili kujipima yale waliyojifunza kupitia uwepo wa maonesho hayo.
Pinda amesema ni lazima kupima athari chanya za maonesho hayo kwa jamii kwani ipo athari katika kutokujua matokeo kwa mtu kuja kujionea teknolojia mbalimbali pasipo utaratibu wa kuulizana tija iliyojitokeza ambapo maonesho hayo hufanyika kila mwaka na mwaka huu yamebebwa na na kauli mbiu Agenda ya 10/30 Kilimo ni biashara shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo mifugo na uvuvi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Fatma Mwasa wakati akimkaribisha mgeni rasmi amesema wanatarajia maonesho yajayo tathimini itakuwa ikifanyika kuanzia ngazi ya vijiji waliko wakulima kwa kuonyesha namna kilimo kilivyowakwamua kwa kutoa shuhuda zao.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa