Imebainika kuwa hali ya kibiashara wilayani Kilosa iko chini ya mstari wa umaskini ambapo wastani wa pato la mtu ni shilingi 750 kwa siku hali inayoashiria mzunguko wa kuuza na kununua uko chini unaopelekea pato la wilaya kuwa chini sana licha ya kuwepo kwa fursa mbalimbali zilizopo wilayani ambazo hakuna mtu anayezifanyia kazi.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi amebanisha haa wakati wa kikao cha Baraza la Biashara Wilaya ambapo amesema kuwa pamoja na kuzalisha mazao ya kilimo yanazalishwa lakini yanauza yakiwa hayapo katika mnyororo wa thamani ili kuongeza tija halkadhalika upande wa mifugo kwa asilimia kubwa hali bado ni duni kwani fursa za mifugo zipo ikiwemo biashara za ngozi lakini hakuna anayeshiriki ili kujiongezea kipato.
Aidha Mgoyi ametoa rai kwa TCCIA NA Jumuia ya wafanya biashara(JWT) kujiunga katika vikundi vitakavyosaidia kuwa na viwanda vidovidogo vitakavyosaidia kupata tija na kuongeza kipato kwani fursa za kuwa na viwanda vya aina mbalimbali zipo ikiwamo uanzishwaji wa viwanda kama vya sabuni ambapo malighafi zote zinapatikana hapa hapa wilayani badala ya kuagiza toka nje sambamba na kuitazama fursa uwepo wa reli ya standard gauge kuwa ni fursa adhimu kwani inaweza kutengeneza ajira kwa kuwa wabunifu na kuibua biashara za aina mbalimbali kwani kupitia standard gauge upo uwezekanao mkubwa kuongeza kipato bila kusahau kulipo kodi na tozo stahiki kwa mujibu wa sheria na taratibu.
Aidha katika kikao hicho Katibu wa Kamati ya Uwekezaji Wilaya Karoli Leonce akiwasilisha fursa za uwekezaji na hali ya uanzishaji viwanda vipya ndani ya wilaya kwa kipindi cha 2018 ili kufikia azma ya upatikanaji wa viwanda 37 wilayani ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la kuwa na viwanda ambapo amesema katika sekta ya kilimo uwekezaji unaweza kufanyika katika mazao ya pamba, karanga, alizeti, tumbaku, miwa, mahindi,mbogamboga pamoja na ujenzi wa maghala, huku sekta ya mifugo kukiwa na upatikanaji wa nyama na ngozi, sekta ya elimu ikiwa katika ujenzi wa shule binafsi, nishati upande wa uzalishaji umeme, sekta ya mazingira upande wa usafi na mazingira, sekta ya utalii,sekta ya ardhi ukodishaji wa nyumba
Naye Kaimu Afisa Mipango Wilaya Lwomile Vallence amesema kuwa mpango mkakati wa Baraza la Biashara Wilaya chini ya kaulimbiu uchumi wa viwanda na maisha bora ni kuboresha huduma kwa wateja kwa kuhakikisha 80% ya wafanyabiashara wawekezaji wanaridhika na huduma zitolewazo ifikapo Juni 2020, kuhamasisha uwekezaji wa viwanda ndani ya wilaya ambao utaongeza makusanyo kwa mwaka kufikia 5,000,000 ifikapo Juni 2020 pamoja na kufanya mabadiliko katika sekta ya kilimo na mifugo kwa kuhakikisha zaidi ya 50% ya wakulima na wafugaji wa ndani ya Wilaya wanalima na kufuga kibiashara, tija na masoko ya uhakika ifikapo Juni 2020.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kikundi cha Mary’s kinachojihusisha na usindikaji wa mazao ya mboga mboga, matunda na nafaka Bi Marygrace Ng’unga amesema kuwa ili kuweza kufikia uchumi wa viwanda na maisha bora ipo haja kwa Halmashauri kusaidia kutatua changamoto ya upatikanaji wa vifungashio, mchakato wa kupata nembo ya ubora ya TBS, TFDA pamoja na uwezeshaji wa kifedha.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa