Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa kwa mwaka wa fedha 2019/2021 imejipanga kukusanya jumla ya shilingi 54,320,649,265.80 kutoka katika vyanzo mbalimbali ikiwemo serikali kuu, mapato ya ndani, michango ya wananchi na wahisani.
Hayo yamebainishwa na Afisa Mipango Wilaya Francis N. Kaunda wakati wa uwasilishaji mpango na bajeti kwa mwaka 2019/2020 katika kikao cha baraza la wafanyakazi ambapo amesema katika ugawaji wa asilimia za mapato ya ndani katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo 40% ya mapato zitaelekezwa katika miradi ya maendeleo huku 60% zitaelekezwa katika matumizi ya kawaida.
Katika kikao hicho Kaunda amesema kwa mwaka 2017/2018 yapo mafanikio yaliyopatikana ikiwemo ujenzi wa njia ya kupitia wagonjwa kwenye hospitali ya Wilaya, upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kwa 95%, ongezeko la ufaulu kutoka 52.89% hadi kufikia 63.775% kwa mwaka 2018/2019 kwa elimu ya msingi, usajili wa vikundi 110 vya vijana na vikundi 200 vya wanawake, kukamilika kwa ujenzi na ukarabati wa skimu ya umwagiliaji Lumuma.
Sambamba na hayo Kaunda amesema kuwa Halmashauri imezingatia mpango mkakati wake wa mwaka 2016/2020 uliohuishwa 2017 na kuzingatia mambo mbalimbali ikiwemo kuhimiza maendeleo shirikishi katika ngazi zote pasipo ubaguzi wowote, ushirikishwaji wa wadau katika kubuni vyanzo vipya vya mapato, kushawishi wawekezaji kwa kuboresha miundombinu katika maeneo yenye fursa za uwekezaji, kuendeleza mnyororo wa thamani kwa zao la mpunga, mahindi, alizeti na mazao mengine ya kilimo.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa