Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Mhe. Wilfred Sumari amesema kuwa katika Kipindi cha robo ya kwanza Julai –Septemba 2024/2025 Halmashauri iliweza kukusanya na kupokea jumla ya Shilingi za kitanzania (18,235,984,740.77 )Bilioni 18,milioni 235, laki 984 elfu 740 na senti 77 sawa na asilimia 103.74 ya makadirio ya robo ya kwanza ambayo ni sawa na asilimia 25.93 ya makadirio ya mwaka wa fedha 204/2025.
Mhe Sumari amesema hayo wakati akihutubia katika Mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani uliolenga kupitia na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za Halmashauri kwa kipindi cha Robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika 13,novemba 2024.
Amesema kuwa katika kipindi cha Robo ya kwanza 2024/2025 Halmashauri imetumia kiasi cha Shilingi (14,312,161,531.91) Bilioni 14,milioni 312,laki 161 na 531 na senti 91 sawa na asilimia 81.41 ya Makadirio kwa robo ya kwanza na asilimia 20.35 ya makadirio kwa Mwaka wa fedha 2024/2025 ambapo ameendelea kusisitiza Menejimenti kuendelea kusimamia ukusanyaji wa mapato hususan katika vyanzo vipya vilivyoibuliwa kama vile stendi ya Dumila na Mikumi.
Akizungumzia juu ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Mhe Sumari amesema kuwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 Halmashauri imekadiriwa kutumia jumla ya shilingi (17,191,419,359.63) Bilioni 17,milioni 191 na laki 419 na mia 359 na senti 63,katika utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo kati ya Fedha hizo Shilingi (2,240,910,108.80) Bilioni 2, milioni 240,laki 910 na shilingi 108 na senti 80 ni fedha za makusanyo ya ndani ya Halmashauri na shilingi (9,626,353,250.83) Bilioni 9, Milioni 626,laki 353 na mia 250na senti 83 ni fedha za Ruzuku kutoka Serikali Kuu na Shilingi (5,324,156,000.00) Bilioni 5,milioni 324,laki 156 elfu zikiwa ni fedha kutoka kwa Wahisani.
Kwa upande mwingine Mwenyekiti amewataka Wahe. Madiwani kuendelea kuhamasisha Wananchi kujitokeza kwa Wingi Kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kupiga kura na kuwachagua viongozi wanaowataka kwani ni haki yao ya msingi.
Sambamba na hayo amewataka Watendaji wa Kata na Vijiji wakiwa kama wasimamizi wasaidizi wa Kuendelea kuhamasisha Wananchi katika maeneo yao kuona Umuhimu wa kupiga kura na kuchagua viongozi hao wa Muhimu ifikapo 27,Novemba 2024.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilosa amemshukuru Mwenyekiti wa Hamashauri pamoja na Wahe.Madiwani wote kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuisimamia Halmashauri na kuhakikisha kwamba Malengo na dhamira ya Serikali inatimizwa na matokeo chanya kuweza kupatikana.
Aidha ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzani kwa kuleta pesa nyingi za Miradi ya Maendeleo Wilayani hapa hali inayopelekea kupiga hatua katika Nyanja zote ikiwemo Kiuchumi ,Kijamii na Kisiasa.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa