Katika utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Serikali ya awamu ya tano imeipatia Wilaya ya Kilosa kiasi cha shilingi milioni mia sita arobaini na nane kwa ajili ya ukarabati/ ujenzi katika chuo cha Maendeleo wilayani Kilosa ikiwa ni sehemu ya kuinua sekta ya elimu ili kuwaweza watoto wa Wilaya ya Kilosa na nchi nzima kiujumla kujifunza maarifa mbalimbali.
Hayo yamebainishwa Machi 3 mwaka huu na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Asajile Mwambambale wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ambapo amesema kuwa licha ya ujenzi huo wa chuo wilaya imeendelea kufanya miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa wodi mbili ya kina baba na kinamama katika kituo cha Afya Mikumi kupitia mapato ya ndani ambapo pia amesema kuwa wodi ya kinamama katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa imeanza kutumika ambapo kupitia wodi hiyo huduma za afya zitaboreshwa hususan huduma za kinamama.
Aidha amesema kuwa kuhusiana na mwelekeo wa matumizi ya Halmashauri katika matumizi ya fedha zake za mapato ya ndani ambapo Halmashauri ipo katika mgawanyo wa Halmashauri zinazopaswa kutumia asilimia 40 ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya shughuli za maendeleo ambapo kwasasa imefikia asilimia 48 ya mapato ya ndani ikiwa ni ziada ya 8% hiyo ikionyesha jambo la maendeleo ni la kipaumbele katika Wilaya ya Kilosa.
Sambamba na hayo amesema kuwa Serikali katika kuboresha huduma za afya imeipatia Halmashauri magari ya dharura mawili yaliyopaswa kwenda hospitali ya St. Kizito ambapo timu ya menejimenti iliazimia kutokana na uwepo wa kituo cha afya cha Mikumi magari hayo yamehamishiwa katika kituo cha Afya Mikumi ili yaweze kuwasaidia wananchi wa maeneo hayo.
Aidha ameonyeshwa kusikitishwa kwake na lugha ambazo zimekuwa zikitumika kuhusiana na fedha ambazo zilikusanywa kupitia mashine za POS jambo ambalo lilijitokeza 2016 na ambapo Halmashauri imekuwa ikilishughulikia kwa muda mrefu na kwamba kwa nafasi ya ukurugenzi amekuwa akilifatilia ambapo hadi sasa mambo yaliyobainika ikiwemo kuonekana fedha hizo kuchukuliwa na kupelekwa benki kwa utambulisho tofauti, baadhi ya viambata kusoma tofauti hivyo kupelekea kushirikisha wataalam toka TAMISEMI ili kupata uhalisia wa deni na hatua kuchukuliwa kwa waliobainika ikiwemo kupelekwa katika vyombo vya sheria.
Sambamba na hayo Mwambambale ameomba jambo hilo la defaulters kuzungumzwa kwa tahadhari sana kwani limekuwa likisemwa tofauti na kusababisha kumchafua Mkurugenzi na Wilaya kiujumla na kwamba si vema kuongea maneno yasiyofaa iwapo mtu hana ushahidi ambapo pia ameuomba uongozi wa Mkoa na Wilaya kutambua kuwa watumishi waliobainika katika deni hilo hatua stahiki zimeanza kuchukuliwa na kuomba nguvu iongezwe kwa pamoja ili kupata fedha hizo kwa ajili ya shughuli za maendeleo.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa