Halmashauri zote za Kanda wa Mashariki zimetakiwa kufanya ukaguzi wa vipando vyao katika mabanda ya Nane Nane ambapo kila halmshauri imepaswa kujipima kupitia halmashauri nyingine ili kuboresha na kuhakikisha vipando hivyo vinakuwa katika hali njema.
Maagizo hayo yametolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kanda ya Mashariki ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh. Adam Malima ambapo ukanda huo unajumuisha mikoa ya Tanga , Morogoro, Pwani na Dare s salaam ambapo ametaka kila halmashauri kuendelea kufanya maandalizi ya vikundi vya wakulima na wafugaji ambao watashiriki katika maeonesho hayo yanayotarajiwa kuanza Agosti 1 hadi 8, 2022.
Aidha katika hicho kilichohusisha ajenda mbalimbali kwa ajili ya maandalizi ikiwemo ajenda ya bajeti ya maonyesho ya NaneNane ambapo kanda ya Mashariki imejipanga kuhakikisha wadau na wananchi wanapata teknolojia na kujifunza mambo mbalimbali ambapo licha ya kikao hicho kamat i ilitembelea vipando na mabanda yote ili kujionea hali halisi ya maandalizi.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa