Imeelezwa kuwa zoezi la utoaji wa chanjo ya surua/Rubella katika Wilaya ya Kilosa lililofanyika kuanzia tarehe 17/10/2014 hadi tarehe 21/10/2019 katika vituo 56 vya kutolea huduma ya mama na mtoto wilayani Kilosa sambamba na utoaji chanjo ya Polio ya Sindano katika Halmashauri imefikia malengo katika utoaji wa chanjo hizo kama inavyotakiwa na Muongozo wa Chanjo wa Taifa.
Hayo yameelezwa na Muuguzi mkuu Wilaya Mwanaisha Chitanda wakati wa utoaji taarifa ya chanjo baada ya kampeni ya kitaifa ambapo amesema kuwa walengwa wa zoezi hilo walikuwa watoto wa umri wa chini miaka mitano kwa upande wa chanjo ya Surua/Rubella miezi 9-59 juku IPV Miezi 18-42 ambapo usambazaji wa chanjo na vifaa ulifanyika kwa kutumia timu zilizokwenda kwenye kanda pia zilitumika kutoa mafunzo kwa Watumishi waliokuwepo kwenye kanda hizo.
Chitanda amesema kuwa katika kufanikisha kampeni hizo yapo mafanikio yaliyojitokeza ikiwemo kufanyika kwa kikao cha Kamati ya Huduma ya Afya ya Msingi Wilaya (PHC) ambacho kilifanyika ili kusaidia kufanya uhamasishaji katika ngazi ya jamii juu ya zoezi la utoaji wa Chanjo ya Surua na Polio ya Sindan, Jumla ya watoa huduma 330 walipewa mafunzo ya utekelezaji zoezi katika kanda 4 (Lumuma, Mikumi, Kilosa Mjini na Dumilapamoja na usimamizi uliofanyika katika vituo vya kutolea chanjo ikiwa ni pamoja na kutatua mapungufu yaliyojitokeza , km chanjo, na vifaa mbalimbali vya kutolea chanjo.
Pamoja na hayo amesema katika zoezi hilo zipo changamoto zilizojitokeza ikiwemo kuchelewa kwa fedha hivyo kufanya kazi ya uratibu wa zoezi hilo kuwa ngumu, baadhi ya maeneo katika Wilaya kutofikika kwa urahisi kutokana na Changamoto za kijiografia, hususani uwepo mvua nyingi katika maeneo ya Lumbiji, Uleling’ombe, Chonwe, Mbamba, Unone, Vidunda na Munisagara.
Wakati huo huo mradi wa WARIDI unaofikia ukomo wake umetoa taarifa ya Utekelezaji wa mradi wa Usafi wa Mazingira katika Halmashauri ya wilaya – Kilosa mradi ulioanza Agosti 25, 2017 na kutarajiwa kuhitimishwa Disemba 31, 2019 ambapo umefanikiwa katika kuteleta mabadiliko katika maeneo mbalimbali kwa kipindi chote ulipokuwa ukitekelezwa wilayani Kilosa
Akieleza mafanikio hayo mdau toka WARIDI Shadaiya Rwehabula amesema miongoni mwa mafanikio hayo ni kaya zenye vyoo zimeongezeka kutoka kaya 89258(90%) hadi kufikia kaya 105147(97.3%). kaya zenye vyoo bora zimeongezeka kutoka kaya 33675 (35.6%) hadi 53111 (49%), kaya zenye vyoo vya asili zimepungua kutoka asilimia 64.4 na kufikia 51, kupungua kwa kaya zisizo na vyoo kutoka kaya 8717 sawa na asilimia 10 ya kaya zote hadi kufikia kaya 2950 sawa na asilimia 2.7, unawaji mikono umeongezeka kutoka kaya 22916 sawa na asilimia 24 hadi kufikia kaya 42259 sawa na asilimia 39. vijiji 72 sawa na 52% kati ya 139 vimefikia lengo la kaya zote kuwa na vyoo katika kijiji .
Mafanikio mengine ni vijiji 52 (74%) kati ya 72 vilivyofikia lengo la kila kaya kuwa na choo katika kijiji vimefanya uhakiki wa ndani , vijiji 52(100%) vilivyofanya uhakiki wa ndani wa ujenzi na matumizi ya vyoo vimefanyiwa uhakiki wa nje na timu ya Mkoa, Halmashauri na WARIDI, vijiji 41 vimefanikiwa kupata madaraja ya usafi vijiji 11 havikufaulu kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo taasisi kutokuwa na vyoo bora, maeneo ya wazi, migahawa, mikusanyiko kutokuwa safi na baadhi ya kaya kuwa na vyoo hafifu sana (mf. Vyoo vya masulphate).
Naye Afisa Afya Wilaya esther Nyabahwera amesema chini ya mradi wa waridi wamejifunza kufanya kazi kama timu katika ngazi zote kwenye uhamasishaji, ufuatiliaji, ukusanyaji wa takwimu, uchukuaji wa hatua za kisheria na maamuzi ya pamoja ili kwenda mbele katika malengo tuliyojiwekea ya kuiweka jamii nzima kuwa na mazingira safi, motisha kwa wakusanya taarifa za usafi wa mazingira kusaidia kupata taarifa kwa wakati na sahihi, umuhimu wa mafunzo rejea kwa wakusanya takwimu za usafi wa mazingira kwa kila robo pamoja na kuboresha usafi wa mazingira ngazi ya kaya,taasisi na maeneo ya jumuiya.
Akihitimisha uwasilishaji wa taarifa zote mbili ya waridi na chanjo Mganga Mkuu wa Wilaya Dokta Halima Mangiri ametoa wito kwa wadau wa afya kuendelea kutoa ushirikiano hasa katika sekta ya afya ili kuhakikisha wilaya kiujumla inakuwa katika hali ya usafi wa mazingira kwa kuhakikisha tunaendeleza mazuri yote na elimu iliyotolewa na waridi sambamba na kushiriki kikamilifu katika shughuli za afya kama vile hamasa katika chanjo na huduma nyingine zinazotolewa katika sekta ya afya, huku akiahidi kufanyiwa kazi kwa mapendekezo yaliyotolewa na washiriki wa vikao hivyo ili kuboresha huduma za afya na usafi wa mazingira.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa