Imebainika kuwa Saratani ya mlango wa kizazi ambayo husababishwa na virusi vya Human Papilloma ina athari kubwa kwa afya ya wanawake ulimwenguni kote. Inakadiriwa kuwa kila mwaka kati ya wanawake 466,000 wanathibitika kuwa na saratani ya mlango wa kizazi, na wengi wao wako katika nchi zinazoendelea,ikiwemo Tanzania.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Chanjo ya kuzuia Saratani ya Mlango wa kizazi ili kutokomeza maambukizi ya saratani ya mlango wa kizazi kwa mabinti wenye umri wa miaka 14, ambapo amesema kuwa kutokana na ukubwa na ugumu wa kugundua tatizo kwa wananchi walio wengi serikali imeona umuhimu wa kuanzisha chanjo hii ili kulinda kundi kubwa lisipatwe na madhara ya ugonjwa huu wa hususani kwa mabinti hawa wenye umri wa miaka 14, ili kuzuia madhara ya ugonjwa kwao kwani isije ikawa kikwazo katika kufikia malengo yao na ndoto zao.
Miongoni mwa viashiria vya ugonjwa huu ni kuanza kujamiana katika umri mdogo,Kuwa na wapenzi wengi,Kuwa na ndoa za mitala,Kuzaa watoto wengi na Uvutaji sigara,Aidha dalili zake ni Kutokwa damu bila mpangilio au kutokwa na damu baada ya kujamiana,Maumivu ya mgongo, miguu na au kiuno,Kuchoka, kupungua uzito, kupungikiwa hamu ya kula,Kutokwa uchafu uchafu wa majimaji uliopauka wa rangi kahawia au wenye damu kwenye uke na Kuvimba mguu mmoja
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto imeanzisha chanjo ya virusi vya HPV ambayo ni salama, haina madhara na inatolewa bila malipo katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya, shuleni na kwenye vituo vya huduma za mkoba, na ili kupata kinga kamili, binti anatakiwa apate chanjo ya HPV mara mbili. Chanjo ya pili anatakiwa aipate miezi sita baada ya kupata chanjo ya kwanza.
Sambamba na hayo katika tukio hilo la uzinduzi wa chanjo hiyo ya saratani ya mlango wa kizazi iliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Kilosa Town iliyohudhuriwa na wazazi, walimu, viongozi wa mashirika ya dini pia wananchi walijitokeza kwa wingi ili kupata elimu ya ugonjwa huo pamoja na kuwaleta watoto wao waweze kupata chanjo hiyo.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa