Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mh. Seleman Jaffo licha ya kutoa pongezi kwa ujenzi wa kituo cha afya Kidodi ametoa agizo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa kuhakikisha ifikapo tarehe 15 Januari 2019 ujenzi wa kituo hicho uwe umekamilika katika mapungufu madogo yaliyosalia.
Jaffo amesema hayo wakati wa ziara yake wilayani Kilosa katika Jimbo la Mikumi aidha ameagiza ujenzi wa Kituo cha Afya Mikumi unaoendelea uwe umekamilika pindi ifikapo 30 Januari 2019 kwani ujenzi huo uko nyuma ya wakati na kusema kwamba eneo la mikumi ni eneo la njia panda na ujenzi wa kituo hicho ni wa kimkakati ili kusaidia watu ambapo ni eneo ambalo ajali wakati wowote hutokea hivyo ni kituo cha msaada kwa watu wengi.
Naye Mbunge wa Jimbo la Mikumi Mh. Joseph Mbilinyi amemshukuru Mheshimiwa Rais wa awamu ya tano kwa ajili ya fedha ambazo zimekuwa zikitolewa kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya wilayani Kilosa na ametumia fursa hiyo kuiomba serikali iendelee kutupia jicho Wilaya ya Kilosa na na majimbo yake hasa katika sekta ya afya ili iweze kutoa huduma nzuri za kiafya kwa wananchi.
Aidha Jaffo katika ziara yake ametembelea mto Ruhembe unaolalamikiwa kwa muda mrefu kupoteza maisha watu hasa kipindi cha mvua ambapo ameahidi kulibeba suala hilo kwa uzito na kwamba ataangalia namna gani ofisi yake itafanya ili kutatua changamoto hiyo.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa