Mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loatha Sanare akiwa katika ziara yake wilayani Kilosa kukagua maendeleo ya utendaji kazi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kwenye utoboaji wa mlima(tanel) yenye urefu wa zaidi ya kilomita moja ameitaka jamii kuacha hulka ya kusikiliza maneno ya uchochezi na yasiyo na kweli ndani yake yanayoendelea katika mitandao ya kijamii kuhusiana na usitishaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayoendeshwa na Serikali ya awamu ya tano.
Sanare amesema kuwa amesikitishwa na maneno ya uzushi na uchochezi yanayoipotosha jamii kuwa ujenzi wa reli ya kisasa(SGR) awamu ya pili kutoka Morogoro hadi Makutoppora hautatekelezwa jambo ambalo si kweli na kwamba mradi huo upo na unaendelea vizuri ambapo pia amewataka viongozi wa kisiasa hususan wa vyama vya upinzani kufika katika mradi huo ili kujionea shughuli za ujenzi zinavyoendelea kwa ufasaha ambapo mpaka sasa mradi huo umekamilika kwa asilimia 30 huku Serikali ikijizatiti katika usimamiaji wa miradi yenye tija kwa jamii.
Naye Mhandisi Ujenzi kutoka TRC ambaye ni msimamizi wa mradi wa SGR Ismail Ahmad Ismail ameishukuru Serikali ya awamu ya tano chini ya Mheshimiwa Rais John Joseph Pombe Magufuli pamoja na jamii kwa ujumla kwa ushirikiano wanaoutoa kwani ushirikiano huo umekuwa chachu ya kufanya kazi kwa kasi licha ya kukabiliwa na changamoto ya mvua lakini pia wameahidi na kuhakikisha wanakamilisha mradi huo ndani ya mkataba unaotarajiwa kwisha Februari 2021.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa