Katibu Tawala Wilaya Yohana Kasitila ameitaka jamii kutambua kuwa kuwa chanjo ya surua rubela na polio ni muhimu kwa afya ya mtoto kwani inamsaidia kumkinga asishambuliwe na magonjwa hayo, hivyo kila mwananchi anao wajibu wa kuhakikisha kila chanjo hiyo inapotolewa watoto wanapata huduma hiyo.
Akizindua kampeni hiyo Oktoba 17 mwaka huu Kasitila amesema utolewaji wa chanjo hiyo ni kampeni ya kitaifa inayofanyika ili kumkinga mtoto na magonjwa ya surua lubela na polio ambayo inatolewa kwa watoto walio na umri wa miezi 9 mpaka miaka mitano ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali ambazo zinapaswa kuungwa mkono kwa huduma mbalimbali za kiafya ambazo zimekuwa zikitolewa.
Kasitila amesema kuwa chanjo hiyo inatolewa bure katika vituo vyote vya serikali vinavyotoa huduma za kiafya na kwamba serikali haitasita kumchukulia hatua mtu yoyote atakayethubutu kumtoza fedha mwananchi ili kupata huduma hiyo.
Pamoja na uzinduzi huo alitoa wito kwa wananchi ambao hawajajiorodhesha kutumia siku ya jana tarehe 17/10/2019 ambayo ndio hitimisho la kujiorodhesha kuhakikisha wanajiorodhesha katika daftari la mpiga kura kila mmoja katika eneo lake analoishi ili aweze kuwa na sifa ya kikatiba kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24 mwaka huu kumchagua kiongozi anayefaa ama kugombea nafasi za uongozi.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa