Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Alhaji Majid Mwanga ametoa rai kwa wananchi kuendelea kpanda miti katika maeneo mbalimbali ikiwemo kuendelea kusimamia maeneo yote yenye miti na kuwachykulia hatua wafugaji wote wanaoharibu mazingira kwa kuingiza mifugo maeneo yaliyopandwa miti na kusababisha miti hiyo kutoota.
Rai hiyo imetolewa wakati wa zoezi la upandaji miti lililofanyika katika kata ya Chanzuru ambapo amesema kila mmoja anafahamu thamani ya miti, hivyo ni vema miti yote inayopandwa ikasimamiwa na kukua kama ambavyo imekusudiwa huku akisisitiza upandaji miti pembezoni mwa barabara kuu na barabara zilizopo katika maeneo mbalimbali.
Mwanga amesema zoezi la upandaji miti ni muhimu ambapo ametaka taasisi mbalimbali na shule zote kuendelea kupanda miti huku akisisitiza walimu kutoa elimu na kushiriki katika upandaji miti kwa kila shule kwa kupanda miti ya ya aina zote jambo litakalosaidia utunzaji wa mazingira na kwamba zoezi la upandaji miti ni zoezi endelevu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Kisena Mabuba amesema jukumu la upandaji miti ni la kila Wilaya ambalo likifanywa kwa uhakika linaweza kuondoa kwa kiwango kikubwa tatizo la maji na kwamba vyanzo vyote vya maji katika Wilaya ya Kilosa vina mchango mkubwa katika masuala la maji na upatikanaji wakei nchini na kwamba maeneo yatakayopandwa miti yatunzwe kwa ajili ya upatikanaji wa maji.
Kisena amesema kupitia mradi wa RUWASA na MORUWASA maji yatapatikana ambayo yatakuwa yakiwafikia wananchi, hivyo jukumu la kuilinda miti na kuhifadhi mazingira ndivyo huduma ya maji itavyopatikana kwa wingi kwani kwa sasa maeneo mengi yanatumika maji vya visima ambapo amesema endapo tutapanda miti ya matunda na aina mbalimbali za miti itasaidia uhifadhi wa mazingira huku akishauri wananchi wanaolima milimani kuacha kilimo hicho kwani maji wanayotumia kumwagilia ni ya kitambo kifupi ambapo baada ya muda itasababisha uhaba wa maji.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa WAMIRUVU Martin Kasambala amesema katika kuhakikisha azimio na agizo la Makamu wa Rais la upandaji miti linatekelezwa ipasavyo WAMIRUVU imekabidhi miche ya m iti katika maeneo mbalimbali ikiwemo shule ya Sekondari Kilosa iliyopatiwa miche 6000, kijiji cha Ilonga kilichopo katika kata ya Chanzuru kikikabidhiwa miche 4000, Chuo cha Maendeleo ya Wananchi miche 2000 na miche 2000 ikitolewa kwa ajili ya mto Mkondoa.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa