Malezi kwa makuzi ya mtoto yana faida kwa maisha ya baadaye ya mtoto hasa katika kumuimarisha kiuchumi na kuboresha maisha yake ikiwemo kuwa na uwezo wa kufikiri na kuchanganua mambo, viungo kufanya kazi vizuri mfano macho na mikono, kusikia na uwezo wa kuongea kiufasaha, pia mtoto kukabiliana na changamoto za ukuaji zinazochangia kusababisha udumavu na kuwa na uboreshaji wa maisha ya mtoto ya baadae kiafya, kielimu, kijamii na kiuchumi.
Hayo yamebainishwa Disemba 23 mwaka huu na Afisa Lishe Wilaya Zaina Kibona wakati wa kikao cha kamati ya lishe na watendaji wa kata ambapo amesema kuwa huduma za makuzi ya awali ya mtoto zinasaidia watoto wenye utapiamlo mkali kuongezeka uzito zaidi na kurudia katika hali ya kawaida kwa haraka zaidi ukilingalisha na wanapopata chakula dawa peke yake ambapo pia inamsaidia mtoto kuwa na uwezo wa kujiamini katika kujieleza, kufanya vizuri katika masomo, kufanya maamuzi sahihi na kukabiliana na changamoto mbalimbali.
Akieleza suala zima la ukuaji wa mtoto kiakili, kijamii, kihisia na kimaadili amesema inasaidia mtoto kuongezeka kwa ufahamu, uwezo wa kufikiri, kutafakari na kutatua matatizo kulingana na umri wake kwani mtoto huanza kujifunza juu ya mazingira anayoishi kwa kutumia milango ya fahamu (kuona, kusikia, kunusa, kuonja na kugusa) huku upande wa kihisia inamsaidia kumwezesha mtoto kuelewa hisia zake na kujifunza namna ya kuzidhibiti.
Kibona amesema mtoto aliye tumboni anaweza kuathirika na msongo wa mawazo ya mama hivyo ipo haja ya wazazi kuwa makini kwa kila wanachokifanya hususani katika kipindi cha ujauzito ikiwemo kuzungumza na mtoto wao tangu akiwa tumboni lakini pia kuzingatia mavazi ya mama mjamzito ambapo anapaswa kuvaa mavazi yatakayomruhusu mtoto kucheza vizuri (yasiyobana), kupumzika na kusaidiwa kazi nzito na wanafamilia wengine sambamba na kuacha vitendo vya ukatili kwa mama mjamzito mfano kupigwa, maneno makali n.k. ambavyo haviruhusiwi hata kidogo.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa