Wito umetolewa kwa wananchi wote kujenga ari na hulka ya kujiletea maendeleo wenyewe kwa kujikita katika shughuli za uzalishaji hasa katika kilimo cha miwa kutokana na uwepo wa mabonde yanayofaa kwa kilimo hicho ikiwemo bonde la ihombwe ambalo linafaa kwa kilimo hicho na kwamba hiyo ni fursa adhimu na yenye tija.
Wito huo umetolewa Mei 21 mwaka huu na Kaimu Afisa Tawala Reginald Simba aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kilosa katika sherehe ya wakulima wa miwa wa bonde la Ihombwe , Kitunduweta, Mhenda na Ilakala sambamba na kuweka jiwe la msingi katika ofisi ya kampuni ya Geoman Cane Estate ltd sherehe zilizokwenda kwa kauli mbiu ya wakati ni sasa tajirika na miwa.
Simba amesema kuwa ili kuweza kuufikia uchumi wa kati ni vema kujikita katika shughuli za uzalishaji mali ambapo serikali ya awamu ya tano inahimiza wawekezaji kuwekeza pamoja na kuanzisha viwanda kwani uwepo wa viwanda katika maeneo yetu ni fursa nzuri sana ya ajira kwa watu mbalimbali
Aidha amempongeza mwekezaji Dkt. George Mlingwa kwa jitihada zake za kuwa bega kwa bega na wakulima wa miwa ambapo mwekezaji huyo anatarajia kujenga kiwanda cha sukari katika eneo la Ihombwe jambo linalotokana na ongezeko la uzalishaji miwa ambapo pia katika juhudi za kuleta maendeleo katika jamii kampuni ya Geoman kwa kushirikiana na kijiji cha Ihombwe imefanikisha ujenzi uliokamiliaka wa darasa la chekechea pamoja na kuchimba visima viwili ambapo kimoja tayari kimeanza kutumika na wananchi kwa maji safi na salama.
Akisoma risala yake mbele ya mgeni rasmi Mkurugenzi wa kampuni ya Geoman Dkt George Mlingwa amesema kuwa katika mazao ya biashara yote duniani hakuna zao lenye faida kubwa kama zao la miwa kwani ni zao lenye faida.
Akizungumzia upande wa uanzishaji kiwanda cha sukari Dkt Mlingwa amesema kuwa kutokana na ongezeko la uzalishaji miwa kampuni ya Geoman inatarajia kuanza ujenzi wa kiwanda cha miwa mwaka huu na kukamilika Juni 2020 na kwamba uwepo wa kiwanda hicho utahamasisha sana kilimo cha miwa na kupelekea tatizo la kupeleka miwa Kilombero kuisha kabisa sambamba na kushuka kwa gharama za usafirishaji ambapo pia miwa hiyo itasagwa ikiwa bado sacrose kubwa.
Sambamba na hayo Dkt Mlingwa amesema kuwa licha ya changamoto ya tatizo la miundombinu duni katika maeneo ya uzalishaji miwa, tatizo la barabara kuu itokayo Kilosa –Mikumi pamoja na upatikanaji wa ardhi ambapo ameomba serikali kuzitupia jicho la karibuchangamoto hizo, kampuni ya Geoman kama mwekezaji imebuni miradi miwili katika kukuza zao la miwa kwa kuwa na mradi wa uwezeshaji unaowezesha wakulima wapya kulimiwa shamba kati ya nusu eka na ekari moja na kupatiwa mbegu ambapo mradi wa pili ni mradi wa ubia ambapo mkulima anaingia ubia na kampuni.
Kutokana na miradi hiyo tunategemea kuwa zao la miwa litalimwa ka kasi kubwa na hadi kufikia 2025 uzalishaji wa mkiwa katika bonde la ihombwe utafikia tani 50,000 za miwa zenye uwezo wa kuzalisha tani 5000 za sukari huku kimapato zinategemewa kupatikana shilingi bilioni tano kwa 2025. Dkt. Mlingwa ameongeza
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa