Akikabidhi mifuko hiyo Januari 30 mwaka huu Kabudi amesema kuwa ameamua kutoa fedha zake binafsi kununua mifuko hiyo lengo likiwa ni kusaidia kufanikisha ujenzi wa vyumba ili wanafunzi waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu waweze kuanza masomo mapema mara baada ya ujenzi kukamilika .
Mh. Kabudi akiteta jambo na Afisa Mipango Wilaya Francis Kaunda
Aidha amewataka wanafunzi hao kusoma kwa bidiii ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao na kwamba atakuwa mstari wa mbele kuwasaidia katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Mwanafunzi Elieza Chibula (katikati) akitoa shukrani zake
kwa mbunge kwa niaba ya wanafunzi wenzake
Kwa niaba ya wanafunzi wenzake Elieza Richard Chibula amemshukuru mbunge wa Jimbo hilo kwa moyo alioonyesha kujitoa kuwasaidia kutatua changamoto hiyo na kumuahidi kuwa watasoma kwa bidii na kufaulu kwa asilimia 100 katika mitihani ya kidato cha nne mwaka huu dhidi ya asilimi 91 ya ufaulu kwa mwaka 2020.
Mtendaji wa Kata ya Mabula Emmanuel Kimario
Kwa upande wake mtendaji wa kata ya Mabula ambaye aliyepokea mifuko kwa niaba ya wananchi wa Mabula Bw Emmanuel Kimario amesema kuwa msaada huo utasaidia kutatua changamoto waliyo nayo kwani shule ina upungufu wa vyumba viwili vya madarasa ambapo ameeleza kuwa tayari wananchi wameshaanza ujenzi kwa nguvu zao na kwamba ujenzi huo utaghalimu kiasi cha shilingi milion 40 fedha itakayotokana na michango ya wananchi huku akiahidi kuwa atahakikisha hadi mwezi wa pili mwishoni madarasa yanakamilika ili mapema mwezi wa tatu wanafunzi ambao bado hawajaanza masomo waweze kuanza masomo yao mara moja .
Wanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Mabula wakisalimiana
kwa furaha na Mbunge wa Jimbo la Kilosa Prof. Kabudi