Mradi wa Mkaa Endelevu umefanikisha kutengwa kwa Misitu ya Hifadhi za Vijiji yenye ukubwa wa hekta 164,392 katika vijiji 41 katika wilaya 7 katika mikoa 3, Kutangazwa katika Gazeti la Serikali Misitu ya Hifadhi ya Vijiji 30 (kupitia GN 688), Kupungua kwa viwango vya ufyekaji na uharibifu wa misitu katika vijiji, Kuboreshwa kwa maisha ya wanavijiji, Vijiji 31 vilipata zaidi ya shilingi bilioni 4.1 kutokana na uvunaji endelevu wa mkaa na mbao katika kipindi cha Desemba 2015 na Novemba 2021, Kati ya mapato hayo, zaidi ya shilingi bilioni 1.7 walipata wazalishaji na zaidi ya shilingi bilioni 2.4 walipata vijiji kutokana na ushuru.
Mafanikio hayo yameelezwa na Meneja mradi wa mkaa endelevu unaotekelzwa na shirika la kuhifadhi misitu ya asili (TFCG) Charles Leonard mbele ya wabunge wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii pamoja na Chama cha Wabunge Marafiki wa Mazingira walipotembelea Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa na kutembelea msimu wa hifadhi katika kijiji cha Chabima kata ya Masanze ambapo amesema wanaomba mapitio ya sera na vipengele vinavyokinzana katika sekta za ardhi, misitu, kilimo, nishati, maji ili kuwepo na uwiano wa kuhifadhi misitu iliyo kwenye ardhi ya vijiji na matumizi mengine ya ardhi,
Aidha wanaomba watunga sera kuunga mkono Usimamizi wa Misitu ya Jamii (CBFM) na kuhamasisha kila Kijiji chenye misitu kutenga eneo kwa ajili ya hifadhi ya msitu wa kijiji, waheshimiwa wabunge kuishauri Serikali kurejesha mamlaka inayotolewa kwa wananchi na Sheria ya Misitu ya Mwaka 2002 zinazotoa mamlaka na wajibu kwa jamii kuhifadhi na kunufaika na rasilimali za misitu kwenye ardhi za vijiji kupitia utekelezaji wa mpango wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu ya Jamii(USMJ) na Biashara endelevu ya mazao ya misitu pamoja na kuishauri Serikali kutojumuisha Misitu iliyoko chini ya USMJ kwenye utekelezaji wa Kanuni za Misitu za Mwaka 2019. (GN. 417) na Watunga sera kutoa kipaumbele katika kuendeleza na kuhamasisha uwekezaji kwenye Usimamizi Shirikishi wa Misitu na uvunaji endelevu wa mazao ya misitu ikiwa ni pamoja na kuongeza thamani ya mazao ya misitu kama nyenzo ya kupunguza upotevu wa misitu kwenye ardhi za vijiji na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Akieleza namna mradi huo unavyofanya kazi amesema mradi huo unalenga kuwezesha Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi ya Kijiji pamoja na kuanzisha Msitu wa Hifadhi wa Ardhi ya Kijiji, Kuhuisha uvunaji endelevu wa mkaa na mbao kwenye Msitu wa Hifadhi wa Kijiji. ~ 10% ya Msitu wa Hifadhi ya Kijiji ni kwa ajili ya uvunaji endelevu wa mkaa ,Kutenga vitalu vya uvunaji: Vitalu vya mita 50x 50., Miti ya mbao haivunwi kwa ajili ya mkaa; Uvunaji hauruhusiwi kwenye vyanzo vya maji; Uoto kujirudia kupita machipukizi na uotaji wa mbegu, Mzunguko w a uvunaji: miaka 24, Teknolojia ya matanuri yaliyoboreshwa na tathmini ya rasilimali ya msitu ili kupata takwimu za uzalishaji.
Kwa upande wa wabunge wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii pamoja na Chama cha Rafiki wa Mazingira wamepokea maombi hayo yaliyowasilishwa kwao huku wakitaka kuongezwa juhudi za kuimarishwa kwa ulinzi wa misitu na kuacha mara moja kuchoma misitu kwani misitu ni uhai na matokeo ya uwepo wa uhai na maji lakini pia kupitia misitu hiyo ni njia ya kupata kipato ambacho kinasaidia kijiji kukidhi mahitaji mbalimbali ikiwemo ujenzi wa kituo cha huduma za afya, ujenzi wa ofisi ya kijiji na matengenezo ya madawati lakini pia wamewahakikishia wananchi hao kuongeza nguvu katika kutimiza ahadi ya Serikali ya kufikisha umeme katika kila kijiji.
Naye mbunge wa Mikumi Mh. Dennis Londo amemshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hasssan kwa kuwezesha huduma ya upatikanaji wa mawasiliano ambayo ilikuwa tatizo kubwa kwa wananchi wa Chabima lakini sasa mawasiliano hayo yanapatikana huku akishukuru kwa ajili ya ujenzi wa kituo kikubwa cha afya unaoendelea katika kata na tarafa ya Masanze ambapo ndio kiktuo cha kwanza cha afya kwa tarafa hiyo, huku Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Kisena Mabuba akiushukuru ugeni huo kwa kuja kuona shughuli zinazofanyika lakini pia ameshukuru uongozi wa TFCG kwa kuwa wadau wakubwa wa utunzaji mazingira huku akiahidi kuendelea kudhibiti wa uwashaji moto holela ili kulinda misitu hiyo.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa