Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango Wilayani Kilosa ikiongozwa na Mweyekiti wake Mhe. Wilfred Sumari ambaye pia ni diwani wa kata ya Chanzuru imefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo ya Halmashauri hiyo lengo ni kuona utekelezaji wa miradi hiyo na hatua zilizofikia kwa wakati uliokusudiwa kukamilika kwa miradi.
Miradi iliyotembelewa ni Pamoja na Jengo la utawala la halmashauri fedha kutoka serikali kuu mradi utaghalimu kiasi cha bilioni 3,200,000, 000 kukamiliaka jengo lipo hatua ya msingi, Ukumbi wa Halmashauri fedha kutoka mapato ya ndani mradi unakadiriwa kiasi cha shilingi milioni 922,627,240 kukamilika ambapo mradi huo upo hatua ya ujenzi wa kuta za boma katika kata ya Mabwerebwere.
Sambamba na Shule ya Sekondari Madoto mradi wa SEQUIP fedha kiasi cha shilingi 528,998,425 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 8, maabara3, jengo la utawala, Tehama, maktaba, matundu ya vyoo 11, kichomea taka na Tank la maji ardhini ambapo ujenzi wa shule hiyo upo hatua ya umalizia katika kata ya madoto.
Pia ujenzi shule ya msingi Mambegwa fedha kiasi cha shilingi milioni 408,900,000 kutoka serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 7, awali 2, jengo la utwala, nyumba ya walimu, matundu ya vyoo 18 pamoja na kichomea taka ujenzi upo hatua ya msingi katika kata ya Msowero.
Aidha Ujenzi wa Shule ya Msingi na Awali Dumila juu mradi wa BOOST kiasi cha shilingi 475,300,000 kwa ajili ya vyumba vya madarasa 14, awali 2, jengo la utawala 1, matundu ya vyoo 18, na kichomea taka ujenzi upo hatua ya umaliziaji katika kata ya Dumila na Umaliziaji wa bwalo shule ya sekondari Berega kata ya berega ambapo miradi hiyo ya shule ikikamilika itawasaidia wanafunzi kutoka umbali mrefu kufata shule pia kupunguza mrundikano wa wanafunzi wengi madarasani.
Mbali na hiyo miradi mingine iliyotembelea na kamati hiyo ni ujenzi wa stendi ya mabasi dumila ambapo chanzo cha fedha ni mapato ya ndani ya halmashauri ikiwa lengo la mradi huo ni kutoa huduma kwa wasafiri kutoka na Kwenda maeneo mbalimbali Pamoja na wanaingia katika kata ya Dumila.
Aidha kamati hiyo imeipongeza serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya wilaya ya kilosa ili kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.
Akiitimisha Ziara hiyo Mhe. Sumari ameipongeza kamati nzima kwa kusimamia vema shughuli za ujenzi zinazoendelea ambapo baadhi ya miradi ipo hatua ya umaliziaji pia ameitaka kamati kuendelea kusimamia baadhi ya miradi yenye changamoto kutafuta utatuzi wa changamoto hizo ili iweze kutekelezeka kwa wakati kama inavyokusudiwa ingawa changamoto nyingi zimetoakana na hali ya mvua zinazoendelea kunyesha kilosa na kukwamisha zoezi kutofanyika kwa wakati.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa