Kamati ya fedha, Uongozi na Mipango ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Mhe. Wilfred Sumari imetembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kipindi cha robo ya pili kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Kamati imetembelea miradi hiyo 03 Februari, 2025, ambapo Wahe. Madiwani wameupongeza mradi wa ukarabarati hospitali ya Wilaya ya Kilosa hususani jengo la maabara ambalo lipo hatua ya umaliziaji na litagharimu kiasi cha shilingi milioni 368 ujenzi huo kukamilika.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mhe. Sumari amesema ameridhishwa na utekelezaji wa mradi huo amao unatekelzwa chini ya mkandarasi AMAL BUILDERS LIMITED na kushauri timu ya wataalamu kwa kushirikiana na wasimamizi wa miradi kutatua changamoto na kufanya marekebisho yanazojitokeza wakati wa utekelezaji wa miradi ili iweze kukamilika kwa wakati na kutoa huduma bora kwa wananchi.
Aidha kamati hiyo ilitembelea na kukagua ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi uliogharimu kiasi cha shilingi milioni150,000,000 ambapo jengo hilo limekamilika kwa asilimia 98 kwa hatua ya umaliziaji.
Miradi mingine iliyotembelewa na kamati hiyo ni pamoja na ujenzi wa ukumbi wa halmashauri, shule ya sekondari kondoa na jengo la madaktari bigwa.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa