Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango Wilayani Kilosa imefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo ya Halmashauri lengo ni kuona utekelezaji wa miradi hiyo na hatua zilizofikia kwa wakati uliokusudiwa.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo 20 Mei, 2024 mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Diwani wa kata ya Chanzuru Mhe. Wilferd Sumari ameipongeza timu ya menejimenti kwa kusimamia vema shughuli za ujenzi zinazoendelea Wilayani hapa huku akiitaka kuendelea kusimamia baadhi ya Miradi yenye changamoto na kuitafutia ufumbazi ili iweze kukamilika kwa wakati kama ilivyokusudiwa ingawa changamoto nyingi zimetokana na hali ya mvua zilizonyesha Wilayani hapa
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Jengo la Utawala la Halmashauri katika kata ya Mabwerebwere fedha kutoka serikali kuu mradi utagharimu kiasi cha shilingi 3,965,145,799.00 kukamilika mpaka sasa mradi upo hatua ya kusimamisha nguzo.
Pia Kamati hiyo imetembelea Ujenzi wa Nyumba ya Mkurugenzi wa Halmashauri iliyopo kata ya Chanzuru. Halmashauri ilipokea kiasi cha shilingi 150,000,000 fedha kutoka serikali kuu ambapo ujenzi upo hatua ya umaliziaji wa kuweka mfumo wa maji safi na maji taka.
Sambamba na shule ya Sekondari Mazinyungu ambapo fedha kutoka serikali kuu kiasi cha shilingi 123,000,000.00 kwa ajili ya vyumba vitano vya madarasa na matundu saba ya vyoo mradi huo uliopo kata ya Mkwatani umekamilika.
Aidha Kamati imetembelea ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Mambegwa iliyopo kata ya Msowero fedha kutoka serikali kuu kiasi cha shilingi 408,900,000 kwa ajili ya jengo la utawala 1, vyumba vya madarasa 7,vyumba vya madarasa ya awali 2, matundu 22 ya vyoo, nyumba ya walimu 2 kwa 1, na kichomea taka.
Mbali na hayo miradi mingine iliyotembelewa na kamati hiyo ni shule ya sekondari Magole kata ya Magole mradi wa SEQUIP fedha kiasi cha shilingi 25,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa ujenzi upo hatua ya umaliziaji pamoja na Ujenzi wa Ukumbi wa Halmashauri uliopo kata ya Mabwerebwere fedha kutoka mapato ya ndani ambapo mradi huo umekadiriwa kutumia jumla ya shilingi 922,627,240.00 na kiasi cha shilingi 266,075,000 zimeshatolewa kutekeleza mradi ujenzi upo hatua ya umwagaji wa zege ya nguzo mlalo ya kwanza.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa