Imeelezwa kuwa matumizi ya mbinu shirikishi kupitia kamati za ulinzi na amani katika vijiji katika kuhakikisha uwepo wa amani katika maeneo mbalimbali hasa kipindi hiki hiki cha mavuno ni mojawapo ya mbinu zinazoweza kusababaisha uwepo wa amani ya kudumu katika vijiji mbalimbali wilayani Kilosa.
Hayo yamebainishwa mwishoni mwa wiki hii na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi wakati wa kikao chake na viongozi wa vijiji vilivyopo katika tarafa ya Masanze kilichokuwa na lengo la kuhakikisha uwepo amani katika kipindi hiki cha mavuno hasa baada ya kuanza kujitokeza viashiria vya uvunjifu wa amani kwa wafugaji kuingiza mifugo katika mashamba ya wakulima.
’’Kila kijiji kinapaswa kuwa na kamati ya amani ambayo itawajibika kuhakikisha uwepo wa amani katika vijiji pamoja na kushirikiana na viongozi wa vijiji katika kutatua kero mbalimbali zinazojitokeza badala ya kusubiri kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ama viongozi wa wilaya’’. Mgoyi ameongeza
Aidha Mgoyi amesema kuwa kila mfugaji anapaswa kuwa na mifugo kulingana na eneo lake pasipo kuvunja sheria na endapo mfugaji atahitaji kupitisha mifugo yake toka kijiji kimoja kwenda kijiji kingine atapaswa kuwa na kibali kitakachomruhusu kufanya hivyo na kwamba atakayekiuka hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Sambamba na hayo amekemea vikali tabia ya wakulima kuuza mabua yakiwa shambani kwani kwa kufanya hivyo husababisha vurugu kwani mifugo licha ya kula mabua yaliyoko shambani ni rahisi kuingia katika mashamba jirani na kula mazao ya watu wengine jambo litakalosababisha uvunjifu wa amani, mapigano pamoja pamoja na upotevu wa mazao kwa wakulima.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa