Ikiwa ni katika msimu wa kuelekea katika maadhimisho ya Siku ya Wakulima Nane Nane kwa mwaka 2022 rai imetolewa kwa viongozi na wataalam mbalimbali kuhakikisha shughuli zote zitakazofanyika zinaendana na jamii ili iweze kujifunza na kupata tija katika shughuli za kilimo, ufugaji na uvuvi.
Rai hiyo imetolewa Juni 29, 2022 na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Martine Shigela wakati wa kikao cha Tathmini ya Maonyesho ya Nane Nane kwa kanda ya Mashariki mwaka 2020 ambapo kikao hicho kilihusisha wakuu wa mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es salaam, wakuu wa wilaya, makatibu tawala mikoa na wilaya, wakuu wa wilaya, wakurugenzi watendaji na wataalam wa kilimo na mifugo pamoja na maafisa habari.
Kwa pamoja wakuu hao wa mikoa wametaka shughuli zote zitakazofanyika kuanzia Agosti Mosi hadi 8 mwaka huu katika viwanja vya Nane Nane mkoani Morogoro, licha ya kuwalenga wakulima na wafugaji lakini pia wananchi wote kiujumla kwa kutoa elimu na teknolojia mbalimbali huku wakisisitiza sekta na wadau wengine kuhusishwa ambapo wameagiza kila Halmashauri kujipanga kuonyesha shughuli zake ikiwemo uwepo wa vipando vya mazao mbalimbali, mifugo na uvuvi huku wakisisitiza taasisi, kampuni na vyuo mbalimbali kuhusishwa.
Aidha kanda ya Mashariki katika maadhimisho ya siku ya wakulima kwa mwaka 2022 imejipanga kufanya maonyesho hayo kuwa bora zaidi kwa kujikita katika kuleta tija kwa wananchi kwa kutoa elimu, ushauri na teknolojia mbalimbali za kilimo, mifugo na uvuvi na masuala mbalimbali ya ujasiriamali ambapo taasisi za kilimo, kidini, utafiti, kibenki na kampuni mbalimbali zitahusika.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa