Wauguzi na wa wakunga wametakiwa kufanya kazi kwa juhudina maarifa kwa wagonjwa wanaofika katika vituo vya afya na hospitali ili kuepusha malalamiko pindi wananchi wanapohitaji kupatiwa huduma za kiafya.
Akizungumza na wauguzi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Morogoro katika siku ya ya Wauguzi Duniani ambayo kimkoa yamefanyika wilayani Kilosa Kaimu Katibu Tawala Mkoa Rosalia Rwegasira amesema kazi ya uuguzi na ukunga ni kazi ngumu inayohitaji imani na huruma katika kutekeleza majukumu yao ambapo siku hiyo huadhimishwa Mei 12 kila mwaka duniani ikiwa ni kutambua kundi hilo ambalo wakati mwingine hutoa muhanga maisha yao ili kuokoa watu wengi.
Maadhimisho hayo yenye kaulimbiu “Wauguzi sauti inayoongoza Wekeza kwenye Uuguzi na Heshimu Haki Kulinda Afya kwa Wote” ambapo amesema siku hiyo ni muhimu kwa wauguzi na wakunga kwani inawakumbusha mambo mbalimbali yanayohusu afya za wanadamu ikiwemo wajibu wwao na wajibu wa wahudumu wa afya katika kufanya kazi kwa kujituma ili kuimarisha afya za wananchi.
Aidha amesema kuwa Serikali inathamini michango ya wauguzi na wakunga katika kutengeneza kada hiyo na kuifanya kuwa ya kutegemewa na wananchi kwa kusaidia kutatua matatizo yanayoihusu jamii huku ambapo katika maadhimsho hayo ambapo uniti 20 za damu ilikusanywa sambamba na kutoa chanjo ya Uviko-19 kwa wananchi watano.
Hata hivyo amesema katika kuadhimisha siku hiyo inaenda sawa na mikakati ya dunia katika kuwekeza kitaaluma kutokana na wanafunzi kujiunga katika vyuo mbalimbali ili kuipata taaluma hiyo huku akiahidi kuzifikisha sehemu husika changamoto zinazowakabili wauguzi na wakunga ili ziweze kutatuliwa.
Akisoma risala kwa niaba katika maadhimisho hayo Edna Bundala ameeleza baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo uhaba wa wauguzi, ukosefu wa sare, vifaa tiba ambapo wameomba Wakurugenzi waruhusiwe kuajiri wauguzi waliopo mitaani.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa