Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe Majid Hemed Mwanga Agosti 27 mwaka huu kwenye mkutano wa hadhara wa kijiji cha Ilonga amejibu kero zanazowakabili wananchi ikiwemo maji na ardhi ambapo amesema kuwa Serikali ina mipango mizuri ya kuwaletea huduma ya maji waliyoikosa kwa muda mrefu kwani tayari milioni 40 zimeshatengwa kwa ajili ya kukamilisha mradi wa maji ya bomba kijijini hapo.
Mh. Mwanga amemtaka Injinia wa Maji Kilosa kuhakikisha pindi mradi wa ujenzi wa kituo cha afya unaoendelea kujengwa ukikamilika pia mradi wa maji uwe umekamilika ili kuondokana na adha ya utumiaji maji yasiyo salama, huku upande wa mgogoro wa ardhi ambao upo kwa muda mrefu amewataka wananchi kuwa na subira kwani suala hilo linafanyiwa kazi ili kuhakikisha wakulima wanapata ardhi kwa ajili ya kuendeleza kilimo.
Katika hatua nyingine amesema kuwa tayari Kamishna wa Ardhi amemuhakikishia kwamba wataalamu watafika Septemba Mosi mwaka huu ili kufanya urasimishaji wa ardhi wa hekari 1400 ambazo zipo katika mgogoro ili kubaini tatizo na kulifanyia kazi.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa