Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Kessy Mkambala amekemea vikali tabia ya baadhi ya wafanyakazi kutowajibika ipasavyo na kutokuwa na nidhamu ya kazi jambo linasababisha maeneo hayo kutokuwa na tija na kusababisha malalamiko kutoka kwa wananchi kwani watumishi wanalo jukumu la kuwatumikia wananchi.
Hayo yamejiri mwishoni mwa wiki hii katika ofisi za Mamlaka ya Mji Mdogo Mikumi wakati mkurugenzi huyo alipokuwa akiongea na watumishi walioko chini ya Mamlaka ya Mji Mdogo kuhusu utendaji kazi wao ambapo amewataka watumishi hao kutogeuza ofisi hizo kuwa kijiwe badala ya kujikita katika kuihudumia jamii inayowazunguka.
Kessy amewataka watumishi wote kiujumla kuwajibika ipasavyo na kuuthibitishia umma wao ni wafanyakazi na wapo ili kuwatumikia ambapo pia amewataka kuhakikisha katikan kipindi hiki cha mavuno mapato yanapatikana hasa katika mazao ambayo wakulima wameshaanza kuvuna.
Sambamba na hayo amemuondolea majukumu aliyekuwa Meneja wa Maji katika Mamlaka ya Mji Mdogo Evance Mombosho na nafasi hiyo kukaimishwa kwa Mtendaji wa Mamlaka ya Mji Mdogo Omary Jaka baada ya meneja huyo kutowajibika ipasavyo katika nafasi yake.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa