Licha yaTahadhari zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali juu ya uwepo wa mvua kubwa za Elnino kutoka mamlaka ya hali ya hewa Nchini, wakazi wa wilaya ya kilosa wanaoishi sehemu za mabondeni na pembezoni mwa mito wameendelea kupewa tahadhari ya kuhama ili kuepusha madhara makubwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Shaka Hamdu Shaka amesema hayo novemba 19,2023 wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua mito na mifereji inayotiririsha maji wilayani hapa na kusema kuwa hali ya mito hiyo pamoja na mifereji ni shwari na hakuna dalili wala viashiria vya mafuriko kama ambavyo inadhaniwa na baadhi ya Watu,hii ni baada ya video fupi kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha mafuriko na mifugo kusombwa na maji jambo ambalo si sahihi.
Mhe. Shaka ameeleza kuwa kamati ya ulinzi na usalama imetembelea na kukagua kwa mito na mifereji inayotiririsha maji na kubaini kuwa kipimo cha maji kwenye mito hiyo ni 0.42 ambacho ni kiwango cha kawaida na kuongeza kuwa wataendelea kufatilia jambo hilo kwa ukaribu lengo likiwa ni kuhakikisha na kuwa Wanachi wa kilosa na mali wako salama.
Mhe Shaka amewaonya Watu wenye tabia ya kutoa taarifa ambazo hawana uhakika kwani zinaweza kuibua taharuki katika jamii na kusabisha hali ya uvunjivu wa amani na usalama kwa wakazi wa eneo husika.
Samba samba na hayo Shaka amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kuipatia Halmasahuri ya Wilaya ya Kilosa fedha kiasi cha shilingi Bilioni 13 kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu za barabara na mifereji ya kisasa inayotiririsha maji na kuizuia kuingia kwenye makazi ya wananchi.
Kwa upande wake Afisa Mazingira wa Wilaya ya Kilosa Ndg. Anthony Heri Mbise amesema kuwa Elimu bado inaendelea kutolewa juu ya kuchukua tahadhali kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali na kuwataka kuchukua taadhali ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.
Mbise ameongeza kuwa vikundi mbalimbali vimeundwa ikiwemo Kamati ya maafa kwa ajili ya kupeana taarifa endapo kuna mabadiliko au viashiria vya kuwepo na mafuriko na kwamba mpaka sasa hakuna taarifa yoyote inayoeleza kuna mabadiliko ya hali ya hewa au mafuriko.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa