Washiriki kutoka Halmashauri ya wilaya ya Kilosa na wadau mbalimbali katika uandaaji wasifu wa Wilaya ya Kilosa wametakiwa kushiriki kikamilifu katika kubaini sekta mbalimbali za uwekezaji wakiwa na taarifa sahihi za sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, ufugaji sambamba na kubainisha ukubwa wa ardhi tuliyonayo kwa ajili ya kilimo na ufugaji kama wilaya.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Asajile Mwambambale ambapo amesema washiriki wanapaswa kutoa taarifa na takwimu mbalimbali wanazozifahamu jambo litakalosaidia zoezi la uandaaji wa mpango wa uwekezaji/ wasifu waWilaya Kilosa chini ya uwezeshaji wa programu ya ENGINE ambao wameleta wataalam washauri (consultants) toka nje na ndani ya nchi ambapo kupitia uwezeshaji wao na taarifa zitakazotolewa zitasaidia kwa kiasi kikubwa kupata mpango wa uwekezaji ili kuitangaza wilaya yetu katika sekta ya uwekezaji.
Aidha amesema kuwa pamoja na kubainisha taarifa na takwimu mbalimbali hususani katika sekta ya kilimo na mifugo pia ametoa wito kwa washiriki hao kutoishia katika kubainisha taarifa hizo bali nao wawe ni sehemu ya kuzitumia sekta hizo badala ya kuwaachia wawekezaji toka nje kwani na wao wana nafasi ya kuwekeza kwani fursa ziyo na inawezekana kuwekeza kwa maslahi yao na wilaya kiujumla.
BAADHI YA WASHIRIKI WA UANDAAJI MPANGO WA UWEKEZAJI
Pamoja na hayo ameeendelea kusisitiza kuwa kazi ya uandaaji mpango wa uwekezaji ni kwa maslahi ya wilaya yetu ili kuweza kuleta tija ambapo amenadi wilaya ya Kilosa ina miji ya Mikumi, Dumila, Ruaha na Kilosa ambayo inaweza kuchangia kukua kwa sekta ya biashara huku akinadi kuwa Wilaya imebarikiwa kuwa na maji mengi ambayo yanaweza kutumika katika kilimo cha umwagiliaji lakini pia uwepo wa ujenzi wa reli ya mwendo kasi (SGR) ambayo Kilosa inatarajiwa kuwa mojawapo ya stesheni kubwa ambapo ametaka uwepo wa stesheni hiyo kutumika kama fursa ya uwekezaji na kwamba uandaaji mzuri wa mpango wa uwekezaji ndio chanzo cha kuvuta wawekezaji kwa wingi zaidi.
BW. ANTONY JONES TOKA KAMPUNI YA AJC MTAALAM WA MIPANGO KATIKA SERIKALI ZA MITAA TOKA MAREKANI
BW. GALINOMA LUBAWA MHADHIRI FEDHA ZA MAENDELEO NA UWEKEZAJI
BW.KELVIN KALEGEYA MWAKILISHI WA PROGRAMU YA ENGINE MKOA WA MOROGORO
Mwambambale pia amewasihi wataalam kutoka ENGINE kwa ajili ya uandaaji wa mpango wa uwekezaji kutosita kuelekeza njia njema ili mchango wao uweze kusaidia mpango wetu kukaa vizuri kwani tuna mambo mazuri yanayoweza kuwa na uwekezaji mzuri na kuitangaza Kilosa kwa ajili ya uwekezaji ikiwemo uwepo wa barabara kubwa ya iliyopita wilayani Kilosa inayounganisha barabarab mbili kubwa za Morogoro - Dodoma mpaka Mwanza na Morogoro - Iringa mpaka Zambia ambayo inapita kutoka Dumila kwenda Mikumi inaweza kuwa kivutio kwa wawekezaji kuona fursa mbalimbali na kuzichangamkia.
.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa