Rai imetolewa kwa wakazi wa Wilaya ya Kilosa kuendelea kujijengea utamaduni wa kufanya usafi na uhifadhi wa mazingira kwani swala la usafi ni afya.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka H. Shaka ametoa Rai hiyo wakati alipozungumza na wananchi mbalimbali waliojitokeza katika maadhimisho ya siku ya usafishaji duniani zoezi lililofanyika katika soko la Mbumi, katika kata ya Mbumi na kwamba swala la usafi linahitaji kupewa kipaumbele sambasamba na kuunga mkono juhudi za serikali katika kuhakikisha mazingira yanakuwa safi.
Akisisitiza suala la usafi Shaka amesema kuwa kwa mujibu wa Sensa ya mwaka 2022, kilosa ina wakazi laki sita na kumi na saba elfu na thelathini na mbili ambao wanazalisha tani 154.3 za taka kwa siku toka vyanzo mbalimbali, hivyo kila mmoja anawajibu wa kuhakikisha Wilaya ya Kilosa inakuwa safi badala ya kusubiri Serikali ifanye kila kitu kwani swala la usafi na uhifadhi wa mazingira ni la kila mmoja wetu.
Aidha amesema kuwa Halmashauri inaendelea na mchakato wa ubinafsishaji wa ukusanyaji taka huku akiwataka wananchi kuunda vikundi vitakavyoomba tenda ya ukusanyaji taka ili kujipatia ajira pamoja na kutunza mazingira kwa kuyaweka safi.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa