Timu ya Kurugenzi FC inayoiwakilisha Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa imerejea nyumbani ikiwa imetwaa kombe la ushindi wa mpira wa miguu SHIMISEMITA kwa kushika nafasi ya pili baada ya kuingia fainali katika mchezo huo zidi ya timu ya Tanga.
Timu hiyo iliyopokelewa kwa furaha 31 Oktoba, 2023 katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa na Mkuu wa Divisheni ya Utawala na Rasilimali watu Betuely J Ruhega amewapongeza kwa juhudi na walizozionesha na kuja na ushindi huo.
Kwa upande wake Afisa wa Utamaduni wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Bi. Paula Katololo amesema kuwa Timu ya kurugenzi FC ni timu imara sana ambayo ilijiandaa vizuri katika michezo hiyo na ameipongeza kwa hatua ya kuingia fainali na kutwa kombe hilo kama washindi wa nafasi ya pili.
Naye Afisa Elimu Ufundi Ahmed Ndimbo ambaye pia alikuwa kocha wa Timu hiyo ameongeza kuwa kurugenzi Fc ni timu bora na anajivunia kuwa kocha wa timu hiyo ambayo imefanya vizuri msimu huu na anaamini itaendelea kufanya vizuri Zaidi katika kipindi kingine.
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmasahuri ya Wilaya ya Kilosa ndg. Kisena Mabuba wakati akipokea kombe hilo Ofisi kwake majira ya asubuhi ameipongeza timu nzima kwa kushiriki mashindano hayo na kurudi na ushindi huo kwa kuiwakilisha vema Wilaya ya Kilosa na kuahidi kuendelea kuwaunga mkono.
Awali SHIMISETA ni Shirikisho la Michezo Serikali za Mitaa iliyofanyika Jijini Dodoma ikiwa na kauli mbiu “Imarisha Afya na Mahusiano Kazini Kwa Maendeleo ya Taifa.”
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa