Katika kupunguza tatizo la udumavu na utapiamlo wilayani kilosa ipo haja ya kutengeneza mpango mkakati wa kukuza rasilimali za kusaidia shughuli za afua za lishe jambo litakalosaidia kupunguza tatizo la udumavu, utapiamlo lakini pia jamii itaelimisha kuhusu tabia bora za lishe ili kuwa na maisha bora kwa kila mwanajamii ifikapo mwaka 2023.
INVIOLATA CHAMI MMOJA WA WAWEZESHAJI WA KIKAO KAZI TOKA KAMPUNI YA DELLOITE
Hayo yamebainishwa Januari 24 mwaka huu na mwezeshaji kutoka kampuni ya Delloite chini ya shirika la USAID Lishe Endelevu Inviolata Chami ambapo amesema lengo la kukutana na kamati ya lishe ni kutengeneza mpango mkakati wa kukuza rasilimali za kusaidia shughuli za afua za lishe kwani mipango ya shughuli za lishe imekuwa haifanyiki kikamilifu kutokana na kukosekana na rasilimali watu, fedha na vifaa hivyo mpango huo utasaidia kamati kutafuta namna ya kupata rasilimali ili kusaidia shughuli hizo.
WASHIRIKI WA KIKAO KAZI WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA
Katika mafunzo hayo wajumbe wa kamati ya lishe walioshiriki katika mafunzo hayo kwa nyakati tofauti wamesema ipi haja ya kubuni vyanzo vipya vya mapato ikiwa ni pamoja na kuanzisha shamba la miwa ya sukari, shamba la ng’ombe wa maziwa , duka la madawa pamoja na kukodisha winchi na malori ya Halmashauri ili kupata fedha lakini pia wamesema kuimarishwa kwa ukusanyaji wa mapato katika vyanzo vya ndani kutasaidia sana ili asilimia tano ya mapato iweze kutolewa kusaidia shughuli za afua za lishe, kufanya mikutano na wadau mbalimbali ili kuweza kuchangia shughuli za lishe ikiwa ni pamoja na kuandaa maandiko kwa wahisani kuongeza nguvu katika shughuli za lishe. Pia wamesema Kilosa uwepo wa changamoto za mafuriko, migogoro ya ardhi, mila potofu na jamii kukosa elimu ya lishe ni miongoni mwa mambo yanayopelekea kushindwa kumudu afua za lishe .
AFISA MIPANGO TUMSIFU KILEO AKIONGEA JAMBO KATIKA KIKAO KAZI CHA KAMATI YA LISHE WILAYA
Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Afisa Mipango Tumsifu Kileo ameishukuru kampuni ya Delloite kwa kikao kazi hicho kwani kimewezesha kutoa mpango kamambe ambao unatoa dira katika kuboresha na kutoa huduma za afua za lishe kuhu akiisisitiza kamati ya lishe wilaya kuwa mstari wa mbele katika kusimamia mpango huo na kuhakikisha unatekelezeka kwa muda uliopangwa.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa