Katika kuendelea kupambana na janga la UVIKO 19 Wilaya ya Kilosa imeendelea kutoa chanjo ya UVIKO 19 kwa wananchi mbalimbali kwa kuhakikisha inawafikia wananchi kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali wa Serikali za vijiji katika maeneo yao.
Akizungumzia namna chanjo hiyo inavyotolewa Afisa Ustawi wa Jamii Bi. Tumaini Geugeu amesema elimu inaendelea kutolewa kwa wananchi juu ya chanjo dhidi ya UVIKO 19 kwa wananchi ambapo licha ya wananchi kutembelewa katika maeneo yao na kupatiwa chanjo hiyo lakini pia inapatikana katika vituo vyote vya afya bure bila gharama yoyote.
Aidha ametoa rai kwa wananchi kutambua kuwa dhamira ya Serikali si kulazimisha watu kuchanja bali kupunguza athari za mlipuko wa ugonjwa huo lakini pia ametaka wananchi kupuuza watu wachache wanaobeza juhudi za Serikali katika mapambano dhidi ya UVIKO 19 kwa kuipotosha jamii kwa maneno yasiyokuwa na ukweli wowote.
Kampeni hiyo ya kutoa chanjo ya UVIKO 19 imeanza tarehe 1/10/2021 na inatarajiwa kuisha 14/10/2021 ambapo tayari kata za Mabwerebwere, Chanzuru, Kimamba, Rudewa na Mkwatani zimeshatembelewa huku kata zilizosalia zikiendelea kutembelewa.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa