Mkuuwa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi amewataka wadau mbalimbali kutochoka kuchangiamichango ya vifaa kwaajili ya kujikinga na janga la corona kwani vifaa hivyobado vinahitajika kwa sababu ugonjwa bado upo na wagonjwa wapo hivyo vitasaidiawataalamu wa afya katika kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.
MKUU WA WILAYA AKIPOKEA MOJA YA VIFAA KUTOKA KWA MMOJA WA WADAU TOKA KAMPUNI YA NAGG GROUP LTD
Mgoyi ametoa rai hiyo Mei 13 mwaka huu wakati akipokea vifaa mbalimbali kutoka kwa kampuni ya NAGG GROUP LIMITED ikiwemo mavazi maalum kwa ajili ya kujikinga na corona(PPE) 9, ngao za uso 5, viatu maalum vya kutolea huduma pea 100 na kofia pea 100.
Hata hivyo Mgoyi amesema awali wadau walikuwa wakichangia kwa ngazi ya tahadhari lakini kwa sasa mchango mkubwa unaohitajika ni wa vifaa kwa ajili kuhudumia wagonjwa kwani kwa sasa wilaya inayo wagonjwa ambapo ili wataalam waweze kutoa huduma kupitia upatikanaji wa vifaa hivyo.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa