Rai imetolewa kwa wananchi kupinga vitendo vya ukatili katikati ya jamii kwani vitendo hivyo vimekuwa vikisababisha madhara makubwa ya kimwili na kiafya kwa jamii kwani ni jukumu la kila mmoja kutoa taarifa pindi anapoona vitendo hivyo vikijitokeza auunapoona mtu akitendewa vitendo hivyo.
Rai hiyo imetolewa na Afisa Maendeleo ya Jamii Bi. Simforosa Mollel wakati wa wa kilele cha siku kumi na sita za kupinga ukatili ambapo zilianza rasmi tarehe 25/11/2022 na kuhitimishwa tarehe 10/12/2022 katika kata ya Magubike ambapo amewata wanakilosa kutambua kuwa ni jukumu la kila mmoja kuungana mkono juhudi za kupinga ukatili huku akisema kuwa chimbuko la siku hizi kumi na sita za kupinga Ukatili dhidi ya Watoto na Wanawake limetokana na wanaharakati ambao walipinga ukatili dhidi ya wanawake uliofanywa na utawala wa kidikteta wa Jamhuri ya Dominika Novemba 25, 1960.
Katika kuhitimisha siku kumi na sita za kupinga ukatili maadhimisho hayo yaliambatana na shughuli mbalimbali yakiwa yamebeba kauli mbiu isemayo KILA UHAI UNA THAMANI TOKOMEZA MAUAJI NA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO ambapo kitaifa yalifanyika Mkoani Tanga huku katika wilaya ya Kilosa yakifanyika katika kata Magubike.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa SMAUJATA Kilosa Mussa Ndekero amewasihi kina baba kuacha kuwanyanyasa akina mama kwani ndiyo watu muhimu kabisa katika familia na kwamba wanapoteseka na kunyanyasika kwa namna yoyote ile inajenga vitendo vya kikatili ambavyo vinapelekea madhara makubwa kwao huku akisema kuwa si kinamaama pekee hufanyiwa vitendo vya kikatili bali hata kinababa hufanyiwa ukatili hivyo ni vema kila mmoja akakemea vitendo vya kikatili.
Kwa upande wao baadhi ya wananchie wamewashukuru sana viongozi wa Serikali na Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa kwa kuhitimishiwa maadhimisho haya ya siku kumi na sita za kupinga Ukatili kwa kupelekewa elimu ya kutosha juu ya kupinga ukatili kwani ni vitendo ambavyo havitakiwi katika jamii tunayoishi na nchi kwa ujumla.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa