Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Bi. Beatrice C. Mwinuka ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia fedha hamashauri hiyo kiasi cha milioni 220 kwa ajili ya ununuzi wa gari jipya la Mkurugenzi.
Bi. Beatrice ameyasema hayo Juni 22, 2025 ofisi kwake bomani wakati akikabidhiwa gari hilo aina ya Toyota Land Cruzer Prado (New Modal) SM 43951 lenye thamani ya shilingi 275 ambapo amesema shilingi Milioni 220 fedha kutoka serikali kuu na milioni 55 fedha kutoka mapato ya ndani.
Mkurugenzi huyo amesema gari hilo litasaidia kupunguza changamoto ya usafiri katika ofisi ya mkurugenzi na pia litaongeza uwajibikaji kwa kuwa gari lililokuwa likitumika awali litatumika katika idara zingine.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa