Uhuru wa Tanganyika sasa Tanzania Bara ulipatikana Desemba 9 mwaka 1961 ambapo mambo makubwa mawili yalifanyika kama sehemu ya maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika ikiwemo kushusha chini bendera ya mkoloni na kupandisha bendera ya Taifa Huru ikiwa ishara ya kumuondoa mkoloni na kupandisha Mwenge wa Uhuru kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halamshauri ya Wilaya ya Kilosa Kisena Mabuba wakati akisoma taarifa ya mafaniko ya wilaya ya kilosa katika kipindi cha miaka 61 ya Uhuru wa Tanznia Bara ambapo amesema kuwa Miaka 61 baada ya Uhuru wa Tanganyika sasa ikifahamika zaidi kwa jina la Tanzania kutokana na Muungano wake na Zanzibar mwaka 1964, ni wakati wa kutafakari na kuona kama taifa hili lipo pahali ambapo wale waliopigania Uhuru walitaka iwe wakati huu na kwamba katika kuenzi siku hii Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa katika kuenzi imefanya shughuli mbalimbali za kijamii ili kuendana na kaulimbiu ya mwaka huu katia miaka 61 ya Uhuru ya “AMANI NA UMOJA NI NGUZO YA MAENDELEO YETU”
Aidha Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa kabla na baada ya uhuru ndani ya miaka 61 imefanikiwa katika sekta ya miundimbinu ya reli na barabara kwani kabla ya Uhuru hatukuwa na miundombinu inayojitosheleza lakini kwa sasa unaweza kutembea kuanzia Kilosa hadi Mwanza na Dar es salaam kwa kutumia barabara ya Lami lakini sasa Wilaya ina mtandao wa barabara zinazohudumiwa na TARURA na sasa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) upo katika hatua za umaliziaji ambapo kutoka Kilosa hadi Dar es salaam itakua inatumia muda wa masaa 2 na kutoka Kilosa hadi Mwanza ni muda wa wastani wa masaa 5.
Upande wa Elimu kabla ya Uhuru elimu ilitolewa kwa upendeleo hasa kwa watoto wa machifu pekee na wanawake walikuwa hawasomi kabisa lakini kwa sasa elimu inatolewa kwa wote bila upendeleo ambapo kabla ya Uhuru Wilaya ya Kilosa ilikua na Shule za Msingi 17 lakini kwasasa ina Shule za msingi 179 za Msingi huku Serikali ikiendelea na Sera ya elimu bure kwa elimu ya awali hadi kidato cha sita huku upande wa Sekondari kabla ya Uhuru kulikua hakuna Shule ya Sekondari lakini sasa tuna jumla ya Shule za Sekondari 47.
Pamoja na mafaniko hayo sekta ya Afya kabla ya Uhuru tulikuwa Hospitali 1 kituo cha Afya 1 na zahanati 6 na baada ya Uhuru ndani ya kipindi cha miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania bara, Wilaya ya Kilosa ina jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya 83 ambapo imepelekea ongezeko la vijiji 68 vilivyo na zahanati kati ya vijiji 138 na kuongezeka kwa idadi vituo vya kutolea huduma kumepunguza ya vifo vya mama na mtoto, kuongezeka idadi ya akina mama wanaojifungulia vituoni na kuboresha huduma za afya ikiwa pamoja na kupunguza umbali kwa wananchi kupata huduma za afya.
Kisena amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa imeendelea kutoa huduma ya Maji safi na Salama kwa wakazi wa Wilaya ya Kilosa kwa upande wa miji ya Kilosa na Mikumi ambapo huduma hiyo hutolewa na Mamlaka ya Maji na usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) huku upande wa Nishati ya Umeme kabla ya Uhuru hapakuwepo na vijiji vilivyokuwa vinapata huduma ya umeme mara baada ya Uhuru katika kipindi cha miaka 61 Wilaya ya Kilosa ina vijiji 75 vimeunganishwa na huduma ya umeme kati ya vijiji 138 na wateja 22,500 wanapata huduma ya umeme.
Licha ya mafanikio hayo katika mawasiliano ya simu, kabla ya Uhuru kulikuwa hakuna mawasiliano yoyote ya simu hasa simu za mkononi, katika kipindi cha miaka 61 ya Uhuru jumla ya vijiji 116 kati ya vijiji 138 vina mawasiliano ya uhakika ya simu za mkononi ambapo minara mbalimbali ya makampuni ya simu imesimikwa katika vijiji kuwezesha Mawasiliano ya kibiashara na kijamii kwa wananchi.
Na katika kuendelea kuhakikisha kuwa Wilaya ya Kilosa inaendelea kuwa mzalishaji bora wa mazao ya Biashara na chakula na kuendelea kuchangia ghala la chakula la Mkoa wa Morogoro kama ambavyo haikuwa kabla ya Uhuru lakini baada ya uhuru Wilaya ya Kilosa imeendelea kuimarisha huduma za ugani kwa wakulima, miundombinu ya kilimo, ambapo kwa sasa jumla skimu 13 ya umwagiliaji zimejengwa na kuboreshwa, Maghala 101 ya kuhifadhia chakula na mazao mengine ya biashara yamejengwa kutoka 7 yaliyokuwepo kabla ya Uhuru na Viwanda vya Kusindika mazao 191 kutoka 5 vilivyokuwepo kabla ya uhuru huku sekta ya Mifugo inaendelea kuimarishwa katika ya miaka 61 ya Uhuru miundombinu mbalimbali ya mifugo imeendelea kuboreshwa ili kuwa na mazingira rafiki kwa Mifugo na wafugaji.
Kutokana na mafanikio hayo Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa inaendelea kumshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuchochea mafanikio haya kwa kuendelea kutoa fedha za kutekeleza miradi maendeleo katika sekta za huduma za Kijamiii, kiuchumi na kuboresha miundo mbinu ya barabara, reli na mawasiliano katika Wilaya yetu ili Wananchi waendelee kupata huduma kwa urahisi na kwa wakati katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa