Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa imekusanya Mapato kiasi cha shilingi Milioni 262 kwa kuuza zao la ufuta kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani.
Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na uvuvi wa halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Ndg. Elia Shemtoi ambapo amesema hadi kufikia Juni 30, 2025 halmashauri imeweza kukusanya kiasi hicho ambacho ni kiwango cha juu ukilinganisha na mwaka uliopita kabla ya kutumia mfumo huo.
Shemtoi ameongeza kuwa mfumo wa stakabadhi ghalani pia umewanufaisha wakulima wengi kwa kupata malipo yao stahiki na kwa wakati, huku akitoa wito kwa wakulima kuupuza taarifa za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya wafanyabiashara kuwa mfumo huo hauna mafanikio.
Aidha Shemtoi amewasihi Maafisa Ugani kuendelea kuelimisha wakulima juu ya umuhimu wa stakabadhi ghalani kwani kupitia elimu watakayoitoa itasaidia kuelimisha na pia kuongeza chachu mabadiliko kwa wakulima.
Pia Shemtoi ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwezesha matumizi ya mfumo huo kupitia wizara ya kilimo kuwa mazao yote yauzwa kupitia mfumo huo lakini pia mfumo wa stakabadhi ghalani umeongeza ajira za muda kwa wananchi katka maeneo ya maghala ambapo kumekuwa na shughuli mbalimbali za maandalizi ya ufuta kabla ya kuhifadhiwa.
Kwa upande wake Afisa Kilimo Mwandamizi mwenye jukumu la kusimamia mfumo huo Ndg. Meshack G. Mkonda amesema kuwa mpaka sasa halmashauri imefanikiwa kuuza mazao jumla ya Tani 3500 katika minada 14iliyofanyika, na wakulima wamepata malipo yao kwa wakati bila changamoto yoyote, huku akiwataka wakulima kupeleka mazao yao katika vyama vya msingi na baadae kupelekwa kwenye ghala kuu kwa ajili ya mauzo.
Naye mkulima wa zao la ufuta Bi. Neema Ndiyu mkazi wa magomeni ambaye pia ni mnufaika wa mfumo wa stakabadhi ghalani amesema mfumo huo ni rahisi na unasaidia kwa kiasi kikubwa kuuza mzao yao kwa bei nzuri na kupata kipato halali tofauti na kipindi cha nyuma.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa