Baraza la Madiwani wilaya ya Kilosa limewapongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa na Mweka hazina Wilaya kwa ufanisi mkubwa waliouonesha katika makusanyo ya mapato kwa kipindi cha miezi mitatu na kufikia zaidi ya asilimia 100.
Wakizungumza baadhi ya madiwani kwa nyakati tofauti katika mkutano wa baraza la madiwani Novemba 18 wamesema kuwa haijawahi kutokea ukusanyaji mkubwa wa mapato katika kipindi kifupi na hiyo imetokea kwa kuwa na ushirikiano mzuri waliouonesha dhidi yao hivyo wananstahili pongezi kwa namna ambavyo wanapambana kuhakikisha mapato yanaongezeka ambayo ndio itakuwa chachu ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Awali akizungumza Mwenyekiti wa Halmashauri Mh.Wilfred Sumari amesema kuwa mapato katika mwaka wa fedha 2022-2023 wa kuanzia Julai hadi Septemba zimekusanywa shilingi bilioni 1.2 sawa na asilimia 109 ambapo kwa makisio kwenye robo hiyo yalikuwa ni shilingi bilioni 1.1 ambapo makusanyo hayo yamevuka malengo yaliyokusudiwa ikiwa ni juhudi kubwa za kiutendaji zilizoonyeshwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Kisena Mabuba na Mweka Hazina wa Wilaya Dismas Mgao kwa usimamizi na maelekezo yenye tija kwa watendaji wao ndio yamefanikisha Halmashauri kukusanya mapato ya ndani kwa kiasi kikubwa hivyo wataona namna ya kuwapongeza ili kuleta ufanisi zaidi.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo amezungumzia suala la kutunza vyanzo vya maji kwani wakulima wamekuwa wakilima katika vyanzo vya maji hivyo amewataka watendaji wakasimamie utunzaji wa vyanzo vya maji kama sheria inavyosema huku akisema kuwa ukatikaji wa umeme mara kwa mara ni kutokana na uharibifu mkubwa unaofanywa na jamii kuharibu vyanzo vya maji.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa