Kuelekea katika Maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani Halmashauri ya Wilaya ya kilosa kwa kushirikiana na Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Ilonga wamefanya Kongamano na Vijana lengo likiwa ni kutoa Elimu ya Malezi kwa Vijana ambao ni wazazi wa baadae ili kutengeneza familia bora.
Kongamano hilo limefanyika katika ukumbi wa FDC Ilonga Mei 14, 2024 ambapo Mratibu wa Maadhisho ya Siku ya Familia Duniani ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii Bw. Maximilian F Ndwangira ameeleza siku hiyo itaadhimishwa kwa kufanya matukio mawili ambayo ni kongamano pamoja na Bonanza la Michezo chuoni hapo lengo ni kutoa Elimu kwa Vijana na kuwajenga waweze kuwa wazazi wazuri wa baadae.
Katika Kongamano hilo wanafunzi wa chuo hicho waliweza kuuliza Maswali na kuchangia mawazo mbalimbali kuhusiana na Mada inayosema “Nini kifanyike katika kukubali tofauti zetu kwenye familia Kuimarisha Malezi ya Watoto.”
Siku ya Familia Duniani Uazimishwa kila Mwaka 15, Mei ambapo kauli mbiu ya Mwaka huu inasema “Tukubali Tofauti Zetu kwenye Familia Kuimarisha Malezi ya Watoto.”
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa